Paris, Ufaransa
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika UNESCO, Mhe. Saidi Othman Yakubu amekutana na ujumbe wa Tanzania kutoka COSOTA ulioshiriki mkutano wa CISAC Regional Committee for Africa (CAF), Paris.
Mhe Balozi Saidi Yakubu amebainisha kuwa: "Tumebadilishana mawazo kuhusu mustakabali wa hakimiliki, matumizi ya Akili Unde (AI), ukusanyaji wa mirabaha na fursa za uchumi wa ubunifu barani Afrika.
Nimefurahishwa kuona wataalamu wetu wakifanya tafiti za Shahada ya Uzamivu (PhD) katika maeneo muhimu ya hakimiliki na usimamizi wa mapato ya wasanii. Tanzania itaendelea kuunga mkono juhudi za kulinda ubunifu na kuhakikisha wasanii wetu wananufaika ipasavyo na kazi zao." Amesema Mhe. Balozi Saidi Yakubu.







No comments:
Post a Comment