Tuesday, June 9, 2026

WAISRAEL NAO WAMERUDI NYUMBANI NGORONGORO


Watalii  zaidi ya 40 kutoka Taifa la Mungu wana wa Israel wamerudi Nyumbani, Kutoka Jerusalem hadi Ngorongoro Tanzania  kuja kujionea maajabu ya Ulimwengu.

Watalii hao  wameshuhudia  maajabu (Wonders) ya uumbaji wa Mungu ikiwemo Kasoko ya Ngorongoro, Bonde la Olduvai na  kupata taarifa kuhusu eneo la Laetoli lenye  Nyayo za Binadamu wa kale.

Watalii hao wakiongozwa na Ellyn Zelikman wamesema kuwa  Ngorongoro imekuwa ndoto ya maisha   na wameamua kujivinjari eneo hilo ili kujionea maajabu ya Dunia.

Wamesema wamezoea  kuona alama za kiroho, Utamaduni wa kisasa wa Mediterania unaozunguka miji mashuhuri na Hifadhi za asili lakini Ngorongoro  imewafanya kufungua ukurasa mpya kwa kuona Simba juu ya miti, Faru pembeni mwa ziwa lenye magadi, Tembo, Nyati, Chui, Ngiri, Pundamilia, Nyumbu na wengineo.

Hifadhi ya Ngorongoro kwa takribani miaka mitano (05) iliyopita imepokea zaidi ya watalii 9,367 kutoka nchini Israel ambapo juhudi za kuongeza watalii wengi zaidi zinaendelea.



No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake