Mtangazaji Diva amezungumza hadharani kuhusu mahojiano yake na Bella, akidai amejaribu kusikiliza pande zote mbili katika sakata linalomhusisha Bella na Sheikh Walid.
Kupitia video aliyopost Instagram, Diva amesema lengo lake lilikuwa kubalansi habari.
"Jana niliongea na Bella usiku kwenye podcast yangu. Nilimuuliza maswali lakini alikwepa. Kama vile anaficha ukweli mwingi. Nikawasiliana na upande wa pili nikapata majibu yote," alisema.
Msingi wa Mgogoro: DNA ya Mtoto
Diva amedai kuwa chanzo kikuu cha mvutano ni suala la kipimo cha DNA.
Kwa mujibu wake, Bella na Sheikh Walid walikuwa ndoa rasmi na walitengana kwa talaka.
"Inasemekana aliolewa na Sheikh Walid. Akapewa talaka. Haikuwa zinaa. Sasa amekuja na mtoto na akiambiwa apimwe DNA anakimbia," alidai Diva.
Ameongeza kuwa kesi iliyokuwa mahakamani ilifutwa baada ya upande wa Bella kutohudhuria siku ya kujadili DNA.
Sheikh Walid: "Ni Mstaarabu Mno"
Kuhusu ukimya wa Sheikh Walid, Diva amesema ni kwa sababu ya heshima.
"Kwani asiongee? Huyo alikuwa mke wake. Anaweka heshima ya kutoongea ubaya wa ndani. Sheikh Walid ni mstaarabu mno. Wallah ni innocent," alisema.
Diva amedai kuwa Sheikh Walid sasa "amejenga ukuta" na amechoka na drama.
Madai Mengine
Katika maelezo yake, Diva pia alidai:
1. Bella alikuwa Mkristo kabla ya kusilimu kwa ajili ya ndoa.
2. Hii ilikuwa ndoa yake ya pili, kwani aliwahi kuolewa Burundi.
"Hitimisho langu ni hili: Mtoto apimwe DNA kwanza. Akubali hilo, ndipo mengine yafuate," alihitimisha Diva.


No comments:
Post a Comment