MOROGORO, Oktoba 7, 2026 | Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imetoa tuzo kwa wanafunzi 13 wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) waliofanya vizuri katika masomo kwa mwaka 2026, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono ubora wa taaluma na kukuza wataalamu wa baadaye katika sekta ya kilimo.Tuzo hizo zimetolewa katika hafla iliyofanyika SUA, ambapo TADB imesisitiza umuhimu wa kutambua na kuhamasisha wanafunzi wanaofanya vizuri, hususan katika taaluma zinazohusiana na kilimo, sekta ambayo ni muhimu katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya TADB katika hafla hiyo, Afisa Rasilimaliwatu Mkuu wa Benki hiyo, Bi. Edna Nyatta, amesema ushiriki wa TADB katika utoaji wa tuzo hizo ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya ushirikiano (MoU) yaliyopo kati ya TADB na SUA.
Amesema kupitia ushirikiano huo, TADB imeendelea kushirikiana na SUA katika kutambua, kuhamasisha na kuunga mkono wanafunzi wanaofanya vizuri, pamoja na kuweka mazingira yanayowawezesha vijana kupata fursa za kujifunza na kujenga uzoefu wa kazi. Bi. Nyatta amewapongeza wanafunzi waliotunukiwa tuzo hizo na kuwataka kuendelea kujifunza, kuwa wabunifu na kutumia maarifa wanayoyapata chuoni katika kutafuta suluhisho la changamoto zinazoikabili Tanzania, hususan katika sekta ya kilimo.
“Tunawapongeza kwa kufanya vizuri. Mafanikio haya yasiishie darasani. Tunawahimiza kutumia elimu, ubunifu na maarifa mnayoyapata kutengeneza suluhisho la changamoto zinazolikabili Taifa, hasa katika sekta ya kilimo,” amesema Bi. Nyatta.
Aidha, Bi. Nyatta amesema TADB imeanzisha mpango wa ‘Learn with Us’, unaolenga kuwapa vijana fursa ya kujifunza kwa vitendo kupitia programu ya mafunzo kwa vitendo (Internship).
Amesema kupitia mpango huo, takribani wanafunzi 10 kutoka SUA tayari wamepata fursa za kufanya mafunzo ya vitendo TADB, huku wanafunzi sita kati yao wakifanikiwa kupata ajira za kudumu baada ya kumaliza mafunzo.
Amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za TADB kuwaandaa vijana kwa soko la ajira kwa kuwapatia uzoefu wa vitendo na kuwaunganisha elimu wanayoipata chuoni na mahitaji halisi ya mazingira ya kazi.
Kwa upande wake, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda, ameishukuru TADB kwa kushiriki katika kutambua na kuwatia moyo wanafunzi waliofanya vizuri.
Prof. Chibunda ameiomba TADB kuendelea kutoa fursa za mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi, akiwemo wanafunzi 13 waliotunukiwa tuzo katika hafla hiyo.
Amesema fursa hizo zitawasaidia wanafunzi kuunganisha elimu waliyoipata chuoni na uzoefu wa vitendo katika mazingira ya kazi, jambo litakalowaandaa zaidi kwa ajira na ujasiriamali katika sekta ya kilimo.
TADB imeipongeza SUA kwa kuendelea kutoa wataalamu wanaohitajika katika sekta ya kilimo na kuahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano na Chuo hicho katika kukuza vipaji, kutoa fursa za kujifunza kwa vitendo na kuwaandaa vijana kwa ajira na ujasiriamali katika sekta ya kilimo.
Ushirikiano huo unaendelea kuakisi dhamira ya TADB ya kushirikiana na taasisi za elimu katika kuwawezesha vijana na kujenga kizazi cha wataalamu wenye uwezo wa kuchochea maendeleo ya kilimo na uchumi wa Tanzania.

No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake