Sunday, March 28, 2010

Mawimbi makali yaathiri juhudi za uokozi


  
Waokoaji wanaendelea na juhudi za kuifikia meli ya kivita ya Korea ya kusini iliyozama katika mazingira ya kutatanisha mnamo siku ya Ijumaa.
Inaaminika kuwa zaidi ya mabaharia arobaini bado wamekwama ndani ya chombo hicho huku familia za mabaharia hao zikisubiri kwa mashaka habari kuhusu majaliwa ya mabaharia.
Jamaa wa mabaharia waliokua kwenye Meli hiyo wamepelekwa kwenye mashua ndogo kuzuru eneo la ajali kushuhudia juhudi za uokoaji zinazofanyika.
Lakini mawimbi makali yameathiri juhudi hizo na kuzidisha majonzi miongoni mwa familia pamoja na makundi ya waokoaji.
Meli hiyo ilizama karibu na eneo linalozozaniwa la mpaka wa baharini baina ya Korea ya kaskazini na ya kusini lakini wakuu wa kijeshi wamesema hakuna dalili kwamba Korea ya kaskazini ilihusika.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake