Waandishi Wetu
WAKATI kampeni za uchaguzi mkuu zikikaribia kumaliza mwezi mmoja, mashambulizi baina ya wagombea yanazidi kuwa makali baada ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa kutangaza nia ya kumpandisha kizimbani mke wa rais, huku Jakaya Kikwete wa CCM alirushia makombora wanachama waliokimbilia upinzani.
Kampeni za uchaguzi zilianza rasmi Agosti 21 na kasi yake ilipunguzwa kutokana na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, lakini sasa zinazidi kupamba moto baada ya vyama vyote kuanza rasmi kuwania tiketi ya kuingia Ikulu, Bunge la Jamhuri ya Muungano, Baraza la Wawakilishi na kwenye mabaraza ya madiwani.
Dk Slaa, ambaye amekuwa akieleza jinsi mke huyo wa rais, Mama Salma Kikwete anavyotumia mali za serikali kumpigia debe mkewe, jana alikwenda mbali zaidi alipotangaza kuwa atamfungulia mashtaka ya kutumia vibaya mali za umma.
Akihutubia wananchi wa Kibara kwenye Jimbo la Mwibara jana, Dk Slaa, ambaye amebobea kwenye sheria, alisema Chadema inafikiria kumfungulia kesi Mama Kikwete dhidi ya matumizi hayo ya mali za umma
No comments:
Post a Comment