Binti kutoka Zimbabwe aliyeshiriki katika onyesho maarufu la televisheni la vipaji nchini Uingereza ametakiwa kuondoka nchini humo kutokana na viza ya familia yake inayomruhusu kisheria kuishi nchini humo kuisha.
Kesi ya Gamu Nhengu mwenye umri wa miaka 18 inafuatiliwa na baadhi ya magazeti ya Uingereza yanaounga mkono kubaki kwa binti huyo nchini Uingereza.
Tokea Mzimbabwe huyo aliposhiriki kwenye hatua za mwanzo za mashindano ya muziki ya X Factor nchini humo, ilikuwa wazi kwamba yeye ni mwimbaji hodari.
Lakini sasa kipindi hicho cha televisheni cha kuwatambua wale wenye vipaji vya uimbaji na kutazamwa na zaidi ya watu milioni 14, kimegubikiwa na tatizo la uhamiaji.
Mama yake Bi Nhengu- Mama Nokutula alitoka Zimbabwe kwenda Scotland kwa masomo.
Lakini majuma kadhaa yaliyopita muda wa viza aliyopewa ilimalizika, na sasa idara ya uhamiaji imeiambia familia yake lazima iondoke Uingereza.
Hilo sio jambo lisilo la kawaida, lakini kwa kuwa Nhengu amepata sifa kubwa kutokana na kushiriki katika kipindi hicho, hii ina maana hali ya familia yake inaangaziwa sana na vyombo vya habari vya Uingereza.
Hali ilikuwa tofauti, kiasi kwamba mwishoni mwa wiki Gamu hakuweza kufuzu hatua ya mashindano hayo ya X Factor.
Lakini idadi kubwa ya wapenzi wa kipindi hicho wameelezea kukasirishwa na matokeo hayo.
Je , aliondolewa kwa kuwa wengine walifanya vyema zaidi, au waandaaji walihofia kwamba huenda wakapata mshindi ambaye huenda angetakiwa kuondoka nchini?
Kwa sasa hivi Gamu anao zaidi ya wafuasi zaidi ya nusu milioni kwenye Facebook , wakitaka arejeshwe kwenye mashindano.
Na sio tu watazamaji wa kipindi cha X Factor: Magazeti mengi ya Uingereza yameangazia sana habari hizo, yakionyesha kuwa upande wa Gamu.
No comments:
Post a Comment