John Mngazija akimfanyika kampeni mgombea ubunge Jimbo la Morogoro mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
KIUNGO mshambuliaji wa zamani wa timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam, John Mngazija, alinaswa na kamera yetu katika mitaa ya Madaraka na Makongoro katikati ya mji wa Morogoro, akimfanyika kampeni mgombea ubunge Jimbo la Morogoro mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni mkurugenzi wa timu ya Simba pia ya Dar es Salaam, Abdulaziz Mohamed Abood.Alipohojiwa na mtandao wetu wetu kuhusiana na tukio hilo, Mngazija alidai kwamba kazi ni kazi na kwamba mradi mkono uende kinywani.
"Aziz Abood ni rafiki yangu amenisaidia mambo mengi licha ya tofauti zetu za Yanga na Simba,hivyo kwa kulitambua hilo nimeona na mimi nimpige jeki katika mchakato huu wa uchaguzi,"alisema mchezaji huyo wa zamani wa Yanga na Nyota Nyekundu
Mngazija akiendelea kumnadi mgombea ambaye pia ni mkurugenzi wa timu ya Simba ya Dar es Salaam, Abdulaziz Mohamed Abood.
No comments:
Post a Comment