"Nguruwe mwenye dhamira" alivyo.
NGURUWE mwenye kilema anaweza asiwe kivutio kwa watalii, lakini Wachina wengi wanafurika nchini mwao kwenda kumwona "kitimoto" ambaye hutembea kwa miguu miwili tu ya mbele.Nguruwe huyo mwenye umri wa miaka 10 hivi sasa ni maarufu kijijini kwake ambapo amepewa jina la ‘Zhu Jianqiang',likimaanisha "Nguruwe mwenye dhamira", likiwa linamfaa mnyama huyo wa ajabu.
Young Zhu Jianqiang ana bahati ya kuwa hai hadi leo kwani alipokuwa mdogo kulikuwa na uamuzi wa kumwua ili kumpunguzia matatizo.
Akiwa katika mienendo yake.
Wang Xihai, mwenye kummiliki Nguruwe huyo, aliliambia gazeti la Telegraph kwamba: "Mke wangu alitaka tumtupe lakini nilikataa. Niliona tumpe fursa tuone kama ataishi, na kweli aliendelea kuishi."
Aliendelea kusema aliamua kumfanyisha mazoezi mnyama huyo baada ya kuzaliwa, na baada ya siku 30 aliweza kutembea akirukaruka.
Pia alisema tangu kuzaliwa kwa nguruwe huyo ambaye hivi sasa ana uzito wa kilo 50, nyumba yake imekuwa ikijaa watu kila siku kwenda kumtazama.
"Siwezi kumwuuza hata kwa bei gani," anasema Wang.
Chanzo:GPL
No comments:
Post a Comment