WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda ametangaza nia kuanzisha kituo cha kulea walemavu wa ngozi mkoani Arusha siku za usoni.
Pinda aliyasema hayo juzi usiku alipokuwa mgeni rasmi katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa na taasisi inayotunza watu wenye ulemavu wa ngozi ya Under the same sun juzi jijini Dar es Salaam.
Alisema kama kiongozi ameona abuni kitu kitakachokumbukwa na watu wote, hivyo ameamua kuanzisha kituo hicho ili kuwasaidia walemavu hao.
“Nimeomba kupewa ekari 50 mkoani Arusha, nimeshazipata na sasa maandalizi yanafanyika ili kukijenga,” alisema Pinda.
Pinda ambaye ametajwa kuwa kiongozi anayeguswa zaidi na matataizo hayo, alieleza jinsi alivyoguswa na matatizo hayo mwaka juzi na kulazimika kutoa machozi Bungeni.
“Kwakweli walinitoa machozi, nilizunguka Kanda ya Ziwa, Mwanza, Shinyanga, Kagera Mara na Tabora, halafu niliporudi Bungeni nililia, kuna mtu alinitonesha kwa kuonyesha kuwa jitihada zote zinazofanywa na serikali ni sawa na bure,” alisema Waziri Mkuu Pinda.
“Kwakweli walinitoa machozi, nilizunguka Kanda ya Ziwa, Mwanza, Shinyanga, Kagera Mara na Tabora, halafu niliporudi Bungeni nililia, kuna mtu alinitonesha kwa kuonyesha kuwa jitihada zote zinazofanywa na serikali ni sawa na bure,” alisema Waziri Mkuu Pinda.
Kwa mujibu wa takwimu za polisi, tangu mauaji hayo yalipoanza mwaka 2007, walemavu 59 wameuawa na tisa wamejeruhiwa.
Pinda alisema alifarijika pale mahakama ilipowatia hatiani wahalifu watatu kwa kuwakuta na hatia na kuwapa hukumu ya kunyongwa.
“Tulizungumza na watu wa mahakama, Jaji mkuu akaongeza kasi ya kusikiliza kesi, tulikamata watu watatu na wakahukumiwa kunyongwa. Kwangu hiyo angalau ilinipa matumaini,” alisema Pinda.
Kabla ya mgeni rasmi kukaribishwa, Mkurugenzi wa habari na masuala ya kimataifa wa taasisi hiyo, Vick Ntetema alitambulisha filamu yake inayoonyesha uchunguzi alioufanya kuhusu mauaji ya albino katika kanda ya ziwa.
Karibu ukumbi mzima ulibubujikwa na machozi huku wengine wakiangua vilio kwa sauti kutokana na picha zilizokuwa zikionyeshwa katika filamu hiyo.
CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment