ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, November 24, 2010

Waliotaka kuteka meli ya jeshi kwenda jela

Watu watano raia wa Somalia wanakabiliwa na kifungo cha maisha jela, baada ya kukutwa na hatia ya kufanya uharamia mwezi Aprili waliposhambulia meli ya kijeshi ya Marekani.
Maharamia
Maharamia wa Kisomali
Waendesha mashitaka wanasema watu hao walishambulia meli hiyo - USS Nicholas -- baada ya kudhani ni meli ya kiraia, na walikuwa wakidai karibu dola 40,000 kama kikombozi.

Lakini mawakili wa Wasomali hao wamesema watu hao walipiga risasi hewani ili kuweza kusikika na walikuwa wakiomba msaada.

Kifungo cha maisha

Hukumu hii ni ya kwanza nchini Marekani kuhusiana na kesi juu ya uharamia kwa karibu miaka 200. Watu hao wanakabiliwa na hukumu ya kifungo cha maisha jela.
Watano hao wamekutwa na hatia ya makosa ya uharamia, kushambulia meli, na kushambulia kwa kutumia silaha hatari.
Maharamia
Maharamia wa Kisomali
Walikamatwa mwezi April, pamoja na wengine waliokamatwa siku chache baadaye katika bahari karibu na Djibouti, baada ya kutuhumiwa kuipiga risasi meli nyingine ya Marekani -- USS Ashland.

Wavuvi

Mawakili wa watu hao wanasema, washukiwa hao ni wavuvi na walikuwa wamelazimishwa na maharamia kushambulia meli hiyo.
Kesi hiyo imefanyika Norfolk katika jimbo la Virginia nchini Marekani, eneo ambalo ni moja ya kituo kikubwa cha meli za kivita duniani na pia bandari ya meli - USS Nicholas.
Wasomali
Maharia katika chombo kidogo
Kwa mujibu wa nyaraka za mahakamani, mwezi Machi, mabaharia watano, wenye umri wa kati ya miaka 20 na 30walisafiri kutoka pwani ya Somalia kwa nia ya kutafuta meli ya mizigo na kiteka.
Meli yao ilikuwa imebeba chakula na mafuta na ilikuwa na vyombo vingine vidogo vya baharini pembeni yake. Waendesha amashitaka wanasema vyombo hivyo vidogo lengo lake ni kushambulia meli. Watu hao walikuwa na silaha na mabomu ya kutumia roketi, wamesema waendesha mashitaka.

Dola 30,000

Kwa mujibu wa nyaraka za mahakamani, moja ya washitakiwa, Mohammed Mohdin Hasan amewaambia wapelelezi kuwa alikuwa ameahidiwa dola 30,000, iwapo wangefanikiwa.
Waendesha mashitaka wamesema; siku nane baadaye, katika bahari ya Hindi, na ikiwa ni usiku, Hasan, Gabul Abdullahi Ali na Abdi Wali Dire walipanda katika moja ya chombo chao cha baharini na kwenda kushambulia meli waliokuwa wakidhani ni ya kiraia na ni ya mizigo.
Maharamia
Wanajeshi wanaofanya doria
Lakini badala yake, meli hiyo ilikuwa USS Nicholas, ambayo ilikuwa imepelekwa katika pwani ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kufanya doria ya kupambana na uharamia.
Hasan na Dire walipeleka chombo chao karibu kabisa na meli ya kijeshi ya Marekani na kufyatua risasi, wamesema waendesha mashitaka. Mabaharia katika meli ya kivita walijibu mashambulizi na kuanza kuwakimbiza na kuwakamata washitakiwa hao, na pia kuteketeza chombo chao.

No comments: