- Usalama wa Taifa wamedhalilishwa
- Ni “uchuro” na fedheha kwa serikali
- Tizameni WikiLeaks. Mtawajua vizuri “rafiki zetu”
Umefika wakati walimwengu wafahamu kwamba mengi katika yale yanayodaiwa na Marekani kuwa ni ugaidi, ni kauli mufilisi na mambo ya kuzua yanayolenga kupumbaza ulimwengu kwa faida ya mabeberu.
Watafiti, wasomi na wachambuzi wa siasa za Marekani wanasema kuwa, kinacholengwa katika “usanii” huo ni manufaa ya kiuchumi, kuhalalisha vita na uvamizi (imperial wars) pamoja na kujenga “dola za kipolisi”.
Pamoja na kuwa maoni haya yamekuwa yakisemwa na waandishi mbalimbali, lakini yameandikwa sana katika masiku ya hivi karibuni kufuatia kile kilichodaiwa jaribio la shambulizi la kigaidi kufanywa na kijana Mohamed Osman Mohamud mwenye asili ya Somalia, lakini ikaja kugundulika kwamba walioandaa hicho kilichokuwa kimedaiwa mipango ya kigaidi ni makachero wa FBI.
Pengine kabla ya kwenda mbali katika kadhia hii ya kijana Osman, tugusie kwanza kidogo juu ya Mtanzania mwenzetu Ahmed Khalfan Ghailan anayeshikiliwa huko Marekani kwa tuhuma kama hizi za huyu kijana wa Kisomali. Katika yanayodaiwa kuwa madai dhidi ya Ghailani, serikali ya Marekani inadai kwamba Ahmed Khalfani Ghailani alinunua vifaa vya kutengenezea mabomu na kuviingiza Dar es Salaam kutoka nchi za nje.
Vifaa hivyo vimetajwa kuwa ni “TNT, detonators, detonation cord, oxygen cylinder tanks na gari la kubebea bomu”.
Baada ya kuviingiza vifaa hivyo nchini, Ghailani anadaiwa alikuwa akipokea wahandisi wa mabomu kutoka nchi za nje ambao aliwatumia kutengeneza bomu na kupanga namna ya kulilipua. Na kwamba bomu lilipokuwa tayari, alikuwa akilihamisha bomu hilo kutoka nyumba moja hadi nyingine katika mitaa ya jiji la Dar es Salaam ili lisigundulike akisubiri siku ya kulipua.
Madai kama haya kwa hakika ni matusi makubwa, dhihaka na kuvidhalilisha vyombo vyetu vya usalama.
Tukirejea kule Oregon, hivi karibuni vyombo vya usalama vya Marekani vilimkamata kijana Mohamed Osman Mohamud (19) kwa madai kwamba alikuwa akitaka kufanya shambulio la kigaidi. Kama ilivyo ada, vyombo vya habari vya Marekani na vipaza sauti vyao mahali pengine, vilikuwa na karamu ya habari siku hiyo. Katika habari yao ya pamoja waandishi William Mall na Nedra Pickler (The Associated Press-Novemba 27, 2010) waliibuka na kichwa cha habari kifuatacho:
“Somali-born teen plotted car-bombing in Oregon.”
Hata hivyo, kulingana na ushahidi uliopatikana ni kuwa kijana huyo hakuwa “gaidi” na kama kuna chochote alichofanya alifanya kwa maelekezo, kusukumwa na kusaidiwa na makachero wa FBI.
“So there was no terror plot, except one hatched and incubated by the FBI, using a would-be surrogate they came across while intercepting internet chatter.”
Alisema mchangiaji mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Jeralyn katika mjadala katika vyombo vya habari baada ya kupatikana habari za kuhusika kwa FBI.
“How long are we going to let the cowboys shoot up our country with false terror plots and operations that would go nowhere without their instigation, planning, and coercion? How long will we allow our own federal constabulary to justify its own recklessly inflated budget by permitting actions like this to develop, fester, and grow operational in our midst?”
“This is terror, pure and simple. State-sponsored terror. Big splash terror designed to make people complaint and fearful, and grateful to their federal government.” Ameandika Teddy.
Akichambua suala hili katika makala yake aliyoipa jina “Fabricating Terror” mwandishi Paul Craig Roberts anasema kuwa kusema kuwa kijana Mohamed Osman Mohamud, mwenye umri wa miaka 19 ni gaidi au alipanga kufanya shambulio la kigaidi ni kupotosha ukweli kwa sababu taarifa za kipolisi zinaonesha kuwa kijana huyo alipewa bomu feki na kachero wa FBI na kupewa maelekezo juu ya nini cha kufanya.
“The Associated Press report by William Mall and Nedra Pickler (11-27-10)… headlined in Yahoo News: “Somali-born teen plotted car-bombing in Oregon” … is a misleading headline as the report makes it clear that it was a plot orchestrated by federal agents. Two sentences into the news report we have this: “The bomb was an elaborate fake supplied by the [FBI] agents and the public was never in danger, authorities said.”
Amesema Roberts akimaanisha kwamba hata katika ile habari ya AP walinukuu kifungu cha taarifa za kipolisi zikikiri kwamba kijana huyo alipewa kinachoitwa bomu na FBI, lakini bado tu AP wakashikilia kusema kuwa kijana huyo alikuwa gaidi hatari.
Taarifa za kiuchunguzi zinaonesha kuwa kijana huyo mwenye asili ya Somalia anayeishi Corvallis, na ambaye ashapata uraiya wa Marekani, alishitakiwa kwamba alifanya jaribio la kuangamiza watu wasio na hatia kwa kutumia silaha za maangamizi (weapon of mass destruction), madai ambayo kama atapatikana na hatia adhabu yake kwa uchache ni kifungo cha maisha.
Maelezo ya awali yanadai kuwa makachero walidai kunasa mawasiliano ya barua pepe (email) ya Mahamud akiwasiliana na mtu aliyepo Pakistan anayetuhumiwa kuwa Al Qaidah na kwamba eti mawasiliano hayo yalikuwa yakionesha kwamba kijana huyo alikuwa na mpango wa kufanya shambulizi la kigaidi. Hiyo ilikuwa baina ya 2007 na 2008.
Habari zaidi zinaonesha kuwa, baada ya FBI kujenga madai hayo waliwasiliana na Mahamud na kuongea naye mambo yaliyohusu “Jihad” na mashambulizi ya kigaidi hadi wakampa mabomu feki ambayo hata yangelipuliwa yasingeweza kulipuka na kuleta athari yoyote. Hayo ndiyo anayodaiwa Mahamud kukamatwa nayo na kudaiwa kuwa yeye ni gaidi.
“The teenager was supplied with a fake bomb and a fake detonator. Friday, an agent (FBI) and Mohamud drove to downtown Portland in a white van that carried six 55-gallon drums with detonation cords and plastic caps, but all of them were inert.”
“They left the van near the downtown ceremony site and went to a train station where Mohamud was given a cell phone that he thought would blow up the vehicle. (However) There was no detonation when he dialed, and when he tried again federal agents and police made their move.”
Inaeleza taarifa moja ikifichua jinsi FBI walivyomtumia Osman kuweka bomu feki na kisha kutuma askari wengine kumkamata na kupaza sauti kwamba kijana huyo alikuwa gaidi.
“FBI walitumia miezi sita kuandaa usanii huu. Wapasha habari wanafananisha usanii huu sawa na uliojulikana kama “the Portland sting” kule Virginia ambapo makachero walimtumia Faroque Ahmed katika njama za shambulizi feki. Ulikuwa ni mpango na zoezi la miezi sita lililoendeshwa na makachero wa serikali kuu.”
Inafafanua taarifa moja ikielezea kiroja hicho cha serikali ya Marekani na kisha kuhitimisha kwa kutoa angalizo lifuatalo:
“Think about this. The FBI did a year”s work in order to convince two people to participate in fake plots.”
Akimaanisha kuwa watu watafakari kwa makini na mazingatio jambo hili ambapo FBI hutumia muda mkubwa (na fedha za walipa kodi) kuandaa mashambulizi ya kigaidi ya kupanga. Hapana shaka muda huu ni kwa ajili ya kuwasomesha nini cha kufanya, kuwalaghai na hata kuwatisha wale inaotaka kuwatumia.
Akielezea matukio kama haya katika makala yake ya Mei 19, 2009 (ambayo ilirejewa kuchapwa Novemba 27, 2010), mwandishi Joe Quinn anaorodhesha matukio ya kupanga (fake plots), na kuelezea jinsi ambavyo watuhumiwa waliteswa hadi kukiri mahakamani au wakati wakihojiwa kwamba walifanya mashambulizi au kupanga wakati si kweli.
“The US government comes up with a plot, an accused, and tortures him until he confesses, or the government fabricates a case and takes it to jurors who know that they cannot face their neighbors if they let off a media-declared “terrorist.”
Hiyo ndiyo Marekani na vita yake ya ugaidi kama anavyoeleza Joe Quinn. Kwamba serikali inapanga ugaidi na kuwatesa inaowalenga ili wakiri kuhusika au wanatumia vyombo vya habari kupiga propaganda kwa hiyo mtuhumiwa huhukumiwa kabla ya kufikishwa mahakamani na hivyo kumjengea hakimu mazingira ya kupitisha hukumu kama serikali inavyotaka.
Lakini nini kinakusudiwa au nini lengo la kufanya usanii huu ambao wakati mwingine hufikia kuwatoa roho watu wasio na hatia? Hili ndilo swali analouliza mwandishi Paul Craig Roberts katika makala yake “Fabricating Terror” pale anaposema, “when the US government has to go to such lengths to create “terrorists” out of hapless people, an undeclared agenda is being served. What could this agenda be?”
Moja ya malengo ama agenda za mipango hiyo anasema Paul kwamba ni kuhalalisha vita vya uvamizi na uporaji wa kibeberu kama ilivyofanyika Iraq na Afgjhanistan. Kama anavyosema Paul, uvamizi wa aina hiyo ni uhalifu. Sasa inachofanya Marekani ni kukwepa kushutumiwa kwa uhalifu wa kivita kwa kujenga mazingira na usanii wa kuonesha kwamba inapambana na magaidi.
“Namna moja ya kuepuka mashitaka ya uhalifu wa kivita ni kubuni ugaidi na kuipakazia nchi unayotaka kuivamia na kuipiga.” Anasema.
Agenda nyingine ni kujenga mazingira ya kuwa na dola la kipolisi (police state) ambapo watu hudhibitiwa na demokrasia kufinyangwa wasiwe na la kuhoji ila kufuata watawala wanavyotaka.
Lakini pia kuna agenda ya kujitajirisha. Ukiacha ule uvamizi na uporaji wa kibeberu kama Marekani inavyofanya Iraq, yapo makampuni ya kibeberu ya Kimarekani ambayo hustawi na kupata faida kubwa kwa kupiga propaganda za kigaidi. Maelezo ni kwamba, ikishapigwa propaganda za kigaidi kwa mfano uliotaka kutokea katika ndege ya abiria ngani au katika uwanja wa ndege, basi sheria za kiusalama zitadaiwa kuboreshwa na kuwa kali zaidi na itapitishwa kwamba ni lazima vyombo vya kuchunguza wasafiri na mzigo yao viongezwe. Na huwekwa kama sheria kwamba uwanja wa ndege usio na vifaa hivyo ndege hazitaruhusiwa kutua. Kisha tenda hutolewa kwa makampuni ya Kiyahudi au Kimarekani kusambaza vifaa hivyo kwa bei watakayo maana hakuna ushindani wa kibiashara. Watu huvuna mapesa kutokana na kitisho walichokibuni wao wenyewe na kwa kushirikiana na makachero wa serikali.
Inatajwa kampuni ya Rapiscan ambayo imepewa tenda ya kusambaza mashine ambayo yaweza kuitwa kuwa ni “full body porno-scanners” kwa viwanja vyote vya ndege, stesheni za treni na mabasi pamoja na maduka makubwa makubwa (shopping malls) huko Marekani. Amri ya kuwekwa kifaa hiki imetolewa baada ya ule usanii wa “underwear bomber” event, ambapo kijana wa ki-Nigeria alidaiwa kutaka kulipua ndege na bomu aliloficha katika chupi. Na ili kuonesha muungano uliopo kati ya makampuni haya ya kibiashara na wanasisa, anatajwa aliyekuwa Mkuu wa Usalama wa Ndani wa Marekani (US Homeland Security), Bwana Michael Chertoff, kwamba ni katika maofisa wa kampuni ya Rapiscan na pia katika wale magwiji wa inayoitwa “Jewish Lobby”.
“The “war on terror” provides an opportunity for a few well-connected people to become very rich. If they leave Americans with a third world police state, they will be living it up in Gstaad.”
Paul Craig Roberts anahitimisha makala yake akionesha jinsi hii inayoitwa vita dhidi ya magaidi inavyotumiwa na wanasiasa na wenye makampuni ya kibeberu kujitajirisha.
Mwandishi Jerry Markon ameandika makala aliyoipa jina “FBI’s use of informants strains ties with Muslims” ndani ya gazeti la Washington Post la Desemba 5, 2010. Katika makala hiyo anaeleza kisa cha Farouk al-Aziz (informant code name Oracle) na (undercover FBI informant) Craig Monteilh ambao walikuwa wakitumiwa na serikali ya Marekani kuhubiri kilichoitwa “violent jihad” katika misikiti, kuwachochea waumini na kuwashawishi kupanga mashambulizi huku wakipiga picha na kunasa mazungumzo yao na Waislamu wakitumia kamera ndogo zinazobanwa kwenye vifungo vya kanzu na vinasa sauti vilivochomekwa kwenye funguo zao walizopewa na FBI.
Anasema katika baadhi ya misikiti na vituo vya Kiislamu waumini wameshawastukia ambapo akija mtu kajivalia kanzu na kuanza kuhubiri “Jihad ya Majambia”, hususiwa na kutimuliwa. Unatolewa mfano kwamba Craig Monteilh alikuwa ametumiwa kuwabambikizia kesi ya ugaidi waumini wa Msikiti na Kituo cha Kiislamu cha Irvine, lakini alikwama.
Inaelezwa katika makala ya Jerry Markon kwamba hivi sasa Monteilh amewashtukia FBI na anataka kuwashitaki. FBI wamekiri kwamba Monteilh ni mtu wao na taarifa zaidi zinaeleza kwamba katika kazi yake aliyofanya kwa muda wa miezi 15, Craig Monteilh amelipwa jumla ya Dola 177,000, (takriban sawa na shilingi 267,000,000 za Kitanzania).
Baada ya kuyasema yote haya, labda sasa tujiulize, watu kama hawa ni wa kuaminika? Watu ambao hadi sasa wanamshikilia Ahmed Khalfani Ghailani kwa tuhuma kama hizi wanazomtuhumu Osman kijana wa Kisomali. Kipi cha kutufanya tusiamini kwamba anachofanyiwa Osman ndicho alichofanyiwa Ghailani?
Viongozi wetu ambao kwa hakika tunawapenda, kuwaheshimu na kuwatii, hawasiti kutukumbusha kwamba wapo maadui wasio kitakia mema “kisiwa chetu cha amani na utulivu.” Sasa hatudhani kwamba “kisiwa hiki” kingeweza kusalimika kwa muda wote huu leo ni miaka 49 ya uhuru iwapo kingekuwa kinaruhusu kuingia wahandisi wa kutengeneza mabomu na zana zao wakatengeneza mabomu mpaka wakayalipua, huku serikali ikiwa haina habari!
Pamoja na umasikini wetu, lakini tunaamini kwamba tuna vyombo madhubuti vya usalama. Haiwezekani yote hayo yakafanyika vyombo vyetu vikiwa kizani. Na hatudhani kwamba vyombo vyetu vimekuwa akina Oracle na Craig Monteilh wanaotumiwa na FBI katika usanii wa “False Flag Terror Operations.”
Hata hivyo yaliyoelezwa hapa ni tone katika bahari. Kuwajua uzuri zaidi rafiki zetu hawa, ingekuwa jambo la kuhimizana kwa kila mmoja wetu kutembelea ile tovuti ya WikiLeaks kujionea mwenyewe yaliyofichuliwa humo.
Amesema kweli Rais Hugo Chavez: “Rafiki zetu” wamevuliwa nguo. “The Empire stands naked.”
Annur
No comments:
Post a Comment