Katika taarifa yake kwa umma jana TCRA imesema wametoa kauli hiyo baada ya kugundua kwamba imezuka tabia ya uvunjaji wa kanuni ya utunzaji wa siri za mawasiliano binafsi ya watumiaji wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi.
Mamlaka imesema kutoa taarifa za mawasiliano binafsi ya simu baina ya watumiaji wa huduma hiyo, ni uvunjaji wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta Na. 3 ya mwaka 2010 na Kanuni za Mawasiliano (Kulinda Wateja) za mwaka 2005.
Mamlaka hiyo imesema adhabu ya kuingilia au kuzuia kupokewa kwa mawasiliano yeyote ya kielektroniki ni faini ya shilingi za kitanzania zisizopungua milioni tano au kwenda jela kwa muda wa usiopungua miaka miwili au adhabu zote kwa pamoja.
Mamlaka imeyataka Makampuni ya simu kuweka uzuizi na kuhakikisha siri za mazungumzo binafsi ya wateja zinahifadhiwa na hazitolewi kwa yeyote isipokuwa kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha yanafanya uchunguzi kugundua walioingilia mazungumzo binafsi ya wateja.
Chanzo:darhotwire
No comments:
Post a Comment