Moja ya hoja ambazo nilizifafanua wiki iliyopita ni kuwa kutoshiriki tendo kwa muda mrefu inaweza kukufanya ushindwe kuonesha kiwango.
Hili kwa wengine huweza kuwa tatizo hasa kwa mtu anayeshindwa kujitambua. Kuna kitu nitakufafanulia.
Umekaa muda mrefu bila kufanya kweli. Hisia zinashamiri ndani kwa ndani matokeo yake siku ya tukio mzigo unamwagika bila hodi.
Hili kwa wengine huweza kuwa tatizo hasa kwa mtu anayeshindwa kujitambua. Kuna kitu nitakufafanulia.
Umekaa muda mrefu bila kufanya kweli. Hisia zinashamiri ndani kwa ndani matokeo yake siku ya tukio mzigo unamwagika bila hodi.
Hatari inayokuja baada ya hapo ni kuwa wengi wetu huanza kujipa mawazo na kusononeka kwa hisia kuwa mtu wake atakuwa amemdharau.
Huyo hata akiitwa kesho, atarudia yale yale. Kumbukumbu za jana zitaendelea kumwathiri na kusababisha aanze kujihisi ni mgonjwa na hana nguvu sahihi.
UNAWEZA KUUMWA KWELI
Mtu anapokabiliwa na mawazo mengi, akidhani anaumwa ugonjwa fulani, kisaikolojia anaweza kuumwa kweli.
Vivyo hivyo, kwa mtu ambaye anadhani ana tatizo la uwezo wa kumudu tendo la ndoa. Huyo mawazo yakikaa kichwani kwake kwa muda mrefu anaweza kuumwa kweli.
Si kwamba atakuwa mgonjwa kwa asilimia 100, bali atafikwa na hali hiyo kutokana na hofu pamoja na kushindwa kujiamini.
Badala ya kuuweka ubongo wake kwenye tendo analotakiwa kulifanya, yeye mawazo yake yanaelekea kwenye kujishtukia, huku akijenga matarajio ya kufeli.
Mawazo huumba. Kushindwa kumudu tendo ni matokeo ya kisaikolojia ambayo unaweza kuyapata, ikiwa ulishindwa kujiamini na ukawa unajishtukia.
NINI CHA KUFANYA
Yapo mengi ambayo unaweza kuyafanya. Kubwa ni wewe mwenyewe kujiamini. Ikitokea ajali mara moja, furahi na ujenge kujiamini kwamba ukirudi mara ya pili utakuwa bora.
Haiwezekani kila siku ikawa Alhamisi. Jenga fikra za ushindi, andaa hisia zako lakini zisizidi kiwango. Aliye mbele yako mwone wa kawaida, tena halali kwa matumizi yako.
PAMBANA NA WOGA
Kinachobeba mantiki ya pointi hii ni kile cha kuogopa ukubwa wa samaki. Kuna mwanafasihi mmoja aliwahi kuimba: “Usiogope ukubwa wa samaki, uliza bei.”
Watu wengine wanapoona warembo wazuri barabarani, hujiangalia kwanza wao na kujitoa kasoro kwa kujiona wapo kiwango cha chini.
Hali hiyo husababisha hata pale unapompata, ushindwe kufanya vizuri mchezo kwa ama kufungia nje au kuwahi mapema kwa sababu ya kuzidiwa na hisia za kutoamini macho yako kama umempata.
Yupo mbele yako, kwa hiyo imani yako ielekee kwenye ukweli kuwa unammudu, hivyo katika mechi ya dakika 90, anaweza kuishia njiani na wewe kufika 120.
Ukijiamini hivyo, bila shaka utaweza pambano. Siku zote amini kuwa woga ni sumu, kwa hiyo pambana ushinde.
AJALI NI MATOKEO
Kama siku ya kwanza mzigo ulikuwa mzito, kwa hiyo uliushusha sebuleni, amini kwamba hiyo ni ajali. Jipange ili mechi nyingine uhakikishe kifurushi unakitua kwenye chumba kinachostahili.
Kuacha mzigo mlangoni ni tatizo ambalo limeshawakuta wengi ambao baada ya kujirekebisha, walikuwa wazuri vile vile.
Achana na wasiwasi, wewe ni bora na hakuna kinachoweza kukushinda ulingoni.
No comments:
Post a Comment