HAPA ni uwanja wetu wa kuzungumza kuhusu mapenzi, kama kawaida na leo pia nitaongelea mambo ya uhusiano. Afya yangu kidogo ina mushkeli, lakini hiyo hainifanyi nishindwe kuzungumza nanyi rafiki zangu. Karibuni sana darasani.
Ni mada ambayo imezaliwa kutoka katika mazungumzo na msomaji wangu kwa njia ya simu. Alinipigia na kuniomba ushauri juu ya tatizo lake, lakini katika maongezi yangu na yeye alionekana kuwa tayari kuendelea kuteswa, kuumizwa, kunyanyaswa katika uhusiano alionao, eti kwa sababu anaogopa kuishi bila mume.
Anataka kuolewa maana anaamini kwamba kutokuolewa ni nuksi! Masikini, alikuwa anawaza tofauti sana. Nilizungumza naye kwa muda mrefu, mwisho akaonekana kuingiwa na kitu fulani cha tofauti. Kilichobaki ni yeye kufanyia kazi ushauri niliompatia.
Hapa nimeona ni vyema kuandika, ili kwa rafiki zangu wengine wenye mtazamo kama wa dada yetu huyo, wabadilike. Naam! Ukimaliza kusoma hapa lazima utabadilika. Twende kwenye mazungumzo yangu na msomaji huyo, ambayo bila shaka yatakupa mwanga wa kuendelea na mada hii vyema.
Alisema yupo kwenye uhusiano na mwanamume ambaye kwake ni kero. Anaeleza kwamba, mpenzi wake huyo ana umri wa zaidi ya miaka 45 na yeye ana miaka 32, wakiwa katika uhusiano huo kwa zaidi ya miaka minne sasa.
Hata hivyo, alisema tatizo kubwa linalouyumbisha uhusiano wao ni kitendo cha mwanamume huyo, kuwa na tabia za kuwatongoza wadogo zake ambao anaishi nao nyumbani kwake. Baada ya kero hizo kuzidi, dada huyo aliona ni bora kuachana naye. Akamweleza mwanamume huyo msimamo wake na kuachana.
Kilichomfaya anipigie simu ni juu ya jamaa huyo kumsumbua kila wakati, akitaka warudiane. Amekuwa akiomba msamaha na kuahidi kwamba hatarudia tena. Alisema, hii siyo mara yake ya kwanza, kwani mara nyingi amekuwa akiwatongoza hata rafiki zake wa karibu na akishtukia mchezo, kazi yake imekuwa kuomba msamaha akiahidi kutorudia lakini baada ya muda, mambo yanakuwa vile vile!
Kinachomuuma zaidi ni kwamba, amejikuta akimpenda sana mwanamume huyo na anashindwa kumuondoa kichwani mwake. Nilizungumza naye juu ya tatizo lake, lakini niliona yawezekana kabisa kuna wengine wengi wenye tatizo kama hilo, lakini hawajui cha kufanya. rafiki zangu, hapa nitakupa njia madhubuti za kutumia ili uweze kukabiliana na tatizo hilo katika uhusiano wako.
Je, upo katika uhusiano na mpenzi ambaye haishi kuwatongoza rafiki, ndugu au watu wako wa karibu? Hapa haijalishi jinsia, nazungumza na wake kwa waume. Dawa hii hapa...
ANABADILIKA?
Siku zote katika uhusiano wowote ule, suala la msamaha ni jema na lenye nafasi kubwa ya kuboresha uhusiano, lakini kabla ya kuchukua hatua ya kusamehe ni lazima ujiulize, anaweza kubadilika?
Hili linaweza kudhibitishwa na historia yake ya nyuma. Haiwezekani ikawa ndiyo mara yake ya kwanza kukosea, lazima atakuwa ameshakukosea mara nyingie huko nyuma.
Je, hili ni kosa lake la kwanza? Alivyokosea huko nyuma aliomba msamaha? Kama aliomba, alirudia tena? Maana kama mtu anakosea kosa lile lile zaidi ya mara tatu na anaomba msamaha akiahidi kubadilika na habadiliki, ujue kwamba si rahisi kubadilika tena!
Lazima ujiridhishe kwamba ni kweli atabadilika na hatarudia tena. Kama nilivyosema hapo juu, utapata ukweli huu kupitia historia yake ya nyuma.
LINGANISHA UMRI NA MAKOSA
Rafiki zangu, kuna aina ya makosa fulani, ukishavuka umri fulani unakuwa huwezi kuyafanya tena, kwa mfano, kesi za kwenda disko na demu mwingine, kwa mwanaume wa miaka 45 huwezi kuzisikia tena.
Sasa hata katika hili, lazima uangalie umri wake kama unafanana na kosa lake. Unajua, kuna tabia nyingine hubadilishwa na wapenzi na nyingine ni za kuzaliwa ambazo kwa hakika huwezi kufanya mabadiliko.
Suala la kubadilisha wapenzi, linaonekana kuwa fasheni zaidi kwa vijana, lakini kama umri wake umeshasonga na bado akawa na tabia hizo, ujue kwamba hiyo ni tabia yake ya asili ambayo haibadilishiki!
Mwanaume wa miaka 52 bado unakimbikizana na vitoto vidogo, lazima kuna tatizo. Wataalamu wa Saikolojia ya Uhusiano na Mapenzi wanaamini wanaume wenye uwezo wa kuwa na familia bora na kuisimamia vyema ni wale wenye zaidi ya miaka 35, kwamba atakuwa ameshapitia mambo mengi na sasa anatamani kuwa baba tu!
Fungua ubongo wako, msimamizi wa familia hawezi kuwa malaya, anatakiwa awe mwenye kujiheshimu. Huyu anafaaa? Wa nini? Akili kichwani mwako.
NI WA MAISHA?
Lakini pia, kabla hujachukua uamuzi wa kuachana naye, lazima ujiulize swali hilo hapo juu, ni mwenzi sahihi wa maisha yako yote? Lazima awe na sifa zitakazomfanya apewe kofia ya mwenzi sahihi.
Rafiki zangu wapenzi, kutokana na ufinyu wa nafasi, naomba kuishia hapo kwa leo, nikikusihi usikose wiki ijayo katika mwendelezo wa mada hii, nitafafanua sifa za mwenzi sahihi pamoja na suluhisho la mwisho la kukabiliana na tatizo hili. SI YA KUKOSA!

1 comment:
OO Babu kumbe unaelewa .inaelekea sasa umekuwa mtu mzima maana .umeandika vitu ,muhimu.
Post a Comment