Neville Meena, Dodoma
SUALA la kifo cha aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk Daudi Balali jana liliibuka bungeni wakati Mbunge wa Mtambile, Masoud Abdallah Salim (CUF), alipoitaka Serikali kutafuta mkanda wa video ili kuuthibitishia umma kuhusu ukweli wa kifo hicho.
“...Serikali inatakiwa itoe tamko kuhusu Balali na kama kweli amekufa basi itoe mkanda wa video kuthibitisha kifo hicho ili isije ikawa historia kama ya Osama Bin Laden alivyozikwa baharini,” alisema Masoud alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Fedha.

Swali kuhusu marehemu Balali limekuja ikiwa imepita miaka mitatu tangu kifo chake kiliporipotiwa kutokea Boston, nchini Marekani alikokuwa amelazwa.Balali alifariki dunia Mei 16, 2008 na kuzikwa huko huko, hali iliyozua mjadala mkali na hisia za tofauti kuhusu ukweli wa kifo hicho.
Desemba 9, 2007, Balali alipokuwa akiendelea na matibabu, aliandikia barua ya kujiuzulu wadhifa kwa Rais Jakaya Kikwete akisema kuwa ni kutokana na sababu za afya yake kuendelea kuzorota na kwamba hakukuwa na dalili za kupona mapema.
Kabla ya Balali kwenda Marekani, sakata la wizi wa fedha za umma kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), hivyo kutokea kwa kifo chake akiwa nje ya nchi kisha kuzikwa huko kulizua gumzo kubwa nchini kuhusu hatma ya tuhuma hizo zilizokuwa zikiwagusa baadhi ya watu wakiwamo vigogo wa BoT.
Jana, Masoud alihoji jinsi Serikali inavyoweza kudhibiti ufisadi wa fedha za umma hali kukiwa na tabia ya kuficha watuhumiwa wengine na baadaye fedha zilizoibwa kutorejeshwa.
Katika kuthibitisha kauli yake, mbunge huyo alitoa mfano wa Dk Balali ambaye kifo chake kiligubikwa na utata na kuelezwa kwamba alifia nchini Marekani, huku akikabiliwa na tuhuma kama hizo.
Kauli hiyo ya Masoud ilisababisha wabunge kuangua kicheko, lakini ikaongoza umakini na usikivu katika Ukumbi wa Bunge, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Gregory Teu aliposimama kujibu swali hilo.
Akijibu swalli hilo, Teu alisema taarifa ambazo Serikali ilizipata kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani zilithibitisha kwamba, Balali alifariki na alizikwa huko huko.
“Taarifa tulizoletewa kutoka kwa balozi wetu nchini Marekani zilieleza Balali alifariki na amezikwa huko huko, hivyo ni kweli Balali hatutamwona tena, amekufa na mambo yote amekufa nayo,” alisema Teu.
Makinda ashangaa mbunge kuuliza swali
Baada ya majibu hayo, Spika wa Bunge, Anne Makinda alieleza kushangazwa kwake na swali hilo kuhusu Balali.
“Mimi nawashangaa sana kwa swali hili, hivi huyu Balali akiwatokea usiku mtasemaje!” alisema Makinda, kisha kuhitimisha kipindi cha Maswali na Majibu bungeni jana.
Mapema akijibu swali la msingi, Teu alisema katika mwaka wa fedha 2009/10, matokeo ya ukaguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali yalibainisha upotevu wa kiasi cha Sh512.477 bilioni ambazo zilikuwa na viashiria vya uzembe, wizi na ubadhirifu.
Katika swali lake, Masoud alitaka kujua kiasi cha fedha ambacho zilihusishwa na uzembe, wizi na ubadhirifu kwa mujibu wa ripoti ya CAG katika kipindi cha Januari 2009 hadi Oktoba 2010 na wahusika walichukuliwa hatua gani.
“....... Matokeo ya ukaguzi yanaonyesha kuwapo na viashiria vya uzembe, wizi au ubadhirifu huwasilishwa kwenye taasisi husika za Serikali zenye mamlaka kwa hatua au uchunguzi zaidi wa kitaalamu na uthibitisho kwa mujibu wa taratibu wa sheria zilizopo,” alisema Teu huku akibainisha kuwa ni vigumu kutoa tamko la moja kwa moja kwamba upotevu huo unatokana na uzembe, wizi au ubadhirifu.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, baada ya kupokea taarifa ya ukaguzi ya mwaka 2009/10, Serikali imeanza kuchukua hatua kwa kufikisha taarifa kwenye vyombo vya uchunguzi, vikiwamo Takukuru na Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua iwapo itabainika kuwapo kwa jinai.

CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment