Mashabiki wa timu ya Yanga wakifanya kitendo ambacho si cha kizalendo kwa kuishangilia timu ya taifa ya Zimbabwe wakati wa mchezo wa kuwania kuingia robo fainali ya michuano ya TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011, uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii na Kilimanjaro Stars kufungwa goli 2-1 . Kitendo hicho kimelaaniwa na hata waandishi wa vyombo mbalimbali vya nje waliokuwa wakiripoti mchezo huo na kusema, "Hii haisaidii maendeleo ya soka na haijawahi kutokea katika nchi zao mashabiki wa nyumbani wakawashangilia wageni".
Mchezaji Thomas Ulimwengu wa Kilimanjaro akijaribu kumtoka Eric Mudzingwa wa timu ya Zimbwabwe katika mchezo wa kuwania kombe la TUSKER CECAFA CHALLENGE CUP 2011 uliofanyika jioni hii kwenye uwanja wa Taifa. Ndani ya dakika 11 timu ya Kilimanjaro Stars imefungwa goli 2 za harakaharaka na timu ya Zimbabwe huku ikishambuliwa kwa muda mdrefu na Wazimbabwe hao hata hivyo katika kipindi cha pili mwishoni timu ya Kilimanjaro Stars imezinduka na kufanikiwa kupata goli 1 katika dakika ya 87 kipindi cha pili. na kufanya matokeo kuwa 2-1 Hivyo kwa matokeo hayo ya 2-1 timu ya Kilimanjaro Stars imefanikiwa kusonga mbele katika hatua ya robi fainali ambapo itashuka dimbani tarehe 6 mwezi huu kucheza na timu ya taifa ya Malawi.
(Picha na maelezo kwa hisani ya FULL SHANGWE)
No comments:
Post a Comment