P.O. Box 21605 Dar Es Salaam -0784-618320/0713-334078/ 0716898685/0658-482597/ 0755067-594
TAARIFA KWA UMMA
Mkutano wa Kilele wa Wanataaluma Tanzania kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru.
Kauli mbiu: Miaka 50 ya Uhuru Mwanataaluma umefanya nini ?
Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN) utawaletea Mkutano wa Kilele wa kwanza wa aina yake kuwakutanisha Wanataaluma ili kuchambua majukumu yao katika kupata ufumbuzi wa vikwazo na katika kuendeleza nchi yetu
Mkutano huu wa Kilele utawakutanisha wanataaluma katika Nyanja mbalimbali, watunga sera,wanasiasa na magwiji wa viwanda ili kujadili majukumu yao ya pamoja katika mjadala wa kujenga na muhimu sana, huku wakiweka bayana majibu ya kuiendeleza nchi mbele
Mkutano huu wa kilele utakuwa na malengo mahususi yafuatayo
· Kutoa uchambuzi wenye lengo la kubainisha mchango wa Wanataaluma au kubainisha mambo ambayo wangefanya katika miaka 50 iliyopita.
· Kutoa uchambuzi wenye lengo la kubainisha iwapo sera za sasa na mifumo ya Kitaifa vitaiwezesha Tanzania kuwa nchi yenye kipato cha kati, kwa kuzingatia zaidi mpango wa MKUKUTA na dira ya nchi kufikia mwaka 2025.
· Kutoa uchambuzi wenye lengo la kubainisha mfumo wa Taifa wa elimu na iwapo una ubora wa kuibadilisha nchi kimaendeleo
· Kujadili kwa kina maswala ya Taaluma na Maadili
· Kuhimiza uhusiano wa karibu zaidi na Watanzania (hasa Wanataaluma) walio nje yaTanzania
Siku hiyo ya Mkutano wa Kilele kutakuwa na shughuli mahususi zifuatazo;
Mada mbalimbali kutoka kwa Watoa mada na Wachangiaji katika mada Nne kama ifuatavyo;
1. Shirikisho la Kikanda: Mgawanyo sawia wa rasiliamali na fursa katika elimu, Biashara na Ajira.
Swali ambalo TPN wangependa kupata majibu kutoka kwa Watanzania ni – “ Je Watanzania wana sifa za kuwawezesha kushindana katika soko la ajira la Kikanda au soko la ajira la Dunia.”?
Kutakuwa na Wachochea mada kuijadili mada yenyewe na kutoa michango yao kabla ya washiriki wote kualikwa rasmi kwenye mjadala.
3. Usimamizi wa Maswala ya Ardhi na Uwekezaji. Je ni kwa kiasi gani Wanataaluma wanapaswa kushawishi sera ya Ardhi na Uwekezaji?
4. Taaluma na Maadili: Uchambuzi wa Faida na Hasara za Kutenda kinyume cha Taaluma na Maadili.
.
5. Je ni mabadiliko gani tunahitaji katika mfumo wetu wa Elimu ili kuwa washindani katika Nyanja ya Dunia?
Mkutano huu wa Kilele unatazamiwa kuzindua tuzo amabayo kila mwaka itatolewa kwa Mtu binafsi Mwanataaluma ili kutambua na kuenzi kazi yake kubwa katika jamii, kwa kuzingatia vigezo kadhaa vitakavyowekwa na Jamii yenyewe.
Kwa mwaka huu Tuzo itakuwa ni kumtambua Baba wa Taifa, Hayati Mwl Julius Kambarage Nyereree kwa msaada wake katika kutumia taaluma yake kuhamasisha watu kupigania Uhuru wa Tanzania na kuhamasisha maendeleo ya taaluma.
Mkutano huu uatfanyika Jumapili tarehe 4-Desemba 2011. Ukumbi : Mlimani City, Muda: Saa 3 Asubuhi – Saa 1 Jioni na Washiriki wa Mkutano Huu Watakuwa watu 500 tu, Kiingilio ni Shillingi 20,000 , lakini kwa Wanachama wa TPN ni Bure !
KUHUSU TPN
Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN) ni mtandao wa hiari, wenye wanachama na usio lenga kupata faida, ambao unalenga kuimarisha nafasi ya Wanataaluma katika kuinua maendeleo ya Jamii ya Watanzania
Jukumu kubwa la Mtandao wa Wanataaluma Tanzania ni ushawishi wa maamuzi yanayofanywa katika ngazi mbalimbali katika sekta ya umma na binafsi kwa njia ya uchambuzi wa mwelekeo wa tafiti zilizopo na matakwa muhimu ya umma.
Kwa maelezo zaidi Wasiliana na :
Katibu Mkuu wa TPN, Mzalendo Janet Mbene
Barua pepe: Maorchid@gmail.com, Simu: +255 784 596444, +255 755 067 594.
Phares Magesa
Rais-Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (TPN)
E-mail: magesa@hotm ail.com
No comments:
Post a Comment