Tarehe 9, December ni sherehe za uhuru wa Tanganyika ambao wengi wetu tumebadilisha na kuita uhuru wa Tanzania. Ni uhuru upi ni swala ambalo tutalijadili siku nyingine. Leo ningependa kuomba tujiangalie sisi Watanzania wa Washington Metropolitan, je tutakuwa wapi December 9, 2011?.
Kwa uhakika kabisa inaonekana Watanzania wa baadhi ya states kadhaa hapa USA kama New York, Delaware, Illinois, nk na nchi nyingi wamejipanga na wengi wao wamejiweka pamoja kama jumuia au kushirikiana na Balozi zao kuadhimisha sherehe za uhuru siku ya tarehe 9, December. Nina uhakika kabisa siku hiyo ya Ijuma wengi wetu tutakuwa makazini tukiwajibika na baadaya hapo tutarejea majumbani bila hata kukumbuka kwamba ni siku ambayo tuliachiwa uhuru wetu wa Waingereza.
Ukiangalia kiundani na kutafakari si kwamba ati sisi si wazalendo wa nchi yetu, na sio kwamba hatutaki kusherherekea sherehe hizi, au kujumuika pamoja bali tumekumbwa na mawimbi ambayo yanatutatiza na yanatufanya tushindwe kuliongoza jahazi letu wenyewe.
Kama Tutakumbuka ni kwamba tarehe 23, September kuliadhimishwa sherehe za uhuru hapa wahington DC, kupitia Ubalozi wetu hapa na Diaspora Council of Tanzanians in America (DICOTA), ambao wengi wetu tulilalama na kuweweseka kwanini sherehe za uhuru zinafanyika September na kwa nini tulipie kwenda kwenye sherehe za uhuru wetu. Malalamiko yetu yalikuwa ya haki kabisa na yakimsingi lakini kwa vile tulikuwa tukisema mmoja mmoja na huku tukiwa nje, tulishindwa kuyafikisha yanako husika, na hatima yake sisi kama wakazi wa hapa tulionekana kuwa tulikuwa wababaifu na tuna puza mazungumzo.(Baseless)
Sasa kongamano la DICOTA lishapita na watu wote pamoja na wageni wa heshima wamerudi makwao na wanajianda kushereherekea sherehe za uhuru haswaa tarehe 9, December. Sie wa DC tupo na tumebaki tunauliza nini kimetokea na inakuwaje tumebaki kwenye hali hii.
Nakubaliana na mawazo ya wengine wanaosema kwamba maisha si yanaendelea kwani tatizo nini ?. Swali langu ni kwamba je sisi kama wana DC tutakubali watu wafanye maamuzi kwa ajili yetu? Wafanye mambo ambayo yanaonekana yamefanywa hapa DC wakati sisi wakazi wa hapa hatukuhusishwa, husika au kukaribia. Wakitengemeza ni kheri , je wakiboronga ? . Tukae tukijuwa kwamba hatuwei kuishi kama mchanga “ Kadri unavyo ubana mkononi ndio unazidi kupungua kupitia vidoleni”
Martin Luther King Says, “Take the First Step. You Don’t Have to See the Whole Staircase, Just Take the First Step”
Wenu mkereketwa
Wa DC
2 comments:
TULISEMA DISEMBA TISA NI UHURU WA TANZANIA, HII NI KUIFANYIA DHAMBI ZANZIBAR, HATA KAMA NI JAMBO DOGO, LAKINI NI LADHAMBI BASI DHAMBI NI DHAMBI TU, HAITAKUWA HAKI KWA MTOTO MDOGO NDANI YA NYUMBA YAKO UKAMDHARAU NA KUMKEBEHI KWA UDOGO WAKE, INAKUWA SIO HAKI NA UNAMDHARAU.
DISEMBA TISA NI UHURU WA TANGANYIKA SIO TANZANIA, TUKISEMA DISEMBA TISA NI UHURU WA TANZANIA TUMESHAITENGA ZANZIA KAMA SIO SEHEMU YA MUUNGANO TULIONAO SASA, TANZANIA NI MUUNGANO WA NCHI MBILI ZENYE MAMLAKA SAWA KISHERIA, KWA WAKATI ULE ZANZIBAR ILIKUWA NA WATU LAKI MBILI NA SITINI ALFU (260,000)PAMOJA NA UCHACHE WA WATU WAKE NA UDOGO WA ENEO ILIKUWA TAIFA KAMILI NA YENYE KITI CHAKE UMOJA WA MATAIFA. TUSIPOTOSHE DHANA YA DISEMBA TISA. SASA TUJIULIZE IKO WAPI TANGANYIKA TUNAYOIADHIMISHA UHURU WAKE, IKIWA TUNASHEREHEKEA UHURU WA TANZANIA, NA ZANZIBAR IKISHEREHEKEA UHRU WAKE, HAPA NI WAZI TABGANYIKA IPO TUSIWE NA NDOTO KWAMBA HAIPO IMEKUBALI KIJIUWA KWA AJILI YA MUUNGANO.
Ndugu Mleta maada.
Ni kwamba zile sherehe za uhuru ziliandaliwa na ubarozi wetu wala si DICOTA ila kwa sababu DICOTA huwa wana utaratibu wao wa kukutana kwa malengo ya kiuchumi na kuleta changa moto za maendeleo, basi ikapendekezwa kwamba hizo shughuli za DICOTA na shughuli za Uhuru zifanyike kwa pamoja na ikapendekezwa kwamba iwe hapa D.C. Lakini hata kama ubalozi ungekuwa haufanyi sherehe za uhuru DICOTA wangefanye mkutano wao wa kiuchumi na biashara kama kawaida. DICOTA imekuwa ikifanya hivi kwa miaka kama mitatu na katika miji mbali mbali na haina matatizo yoyote.
Sisi watu wa D.C kwanza tuna matatizo yetu, kama kukosa umoja, sasa sijui hata kama tukiamua kufanya shughuli nani atakuwa kiongozi ? kwa sababu tuna hitaji sana viongozi, lakini hatujachelewa sana tunaweza tukakutana katika ukumbi wowote hapa D.C tuka shangilia uhuru. Wengine walete vinywaji na wengine chakula -tufanye CHAP-CHAP BASI. WEWE MTOA MAADA PENDEKEZA ENEO NA UWE KIONGOZI WA MUDA...
asante
Post a Comment