Advertisements

Tuesday, April 10, 2012

DC, MD, VA


NDUGU WATANZANIA WA DMV NAPENDA KUWAOMBA RASMI  USHIRIKIANO WENU  KATIKA  ZOEZI HILI LA KUPIGA KURA  LITAKALO FANYIKA 
JUMAPILI  TAREHE 15 APR SAA NANE MCHANA .MIMI LOVENESS NIA KUBWA NI KUTAKA USHIRIKIANO  NA UPENDO KATIKA JUMUIYA YETU NA PIA TUWEZE 
KUSHIRIKIA KWA PAMOJA NA BILA KUWA NA MAKUNDI KWANI  UMOJA NI NGUVU NA UTENGANI NI DHAIFU .TUWE KITU KIMOJA NA KUWEKA NGUZO IMARA .


ENDAPO NITASHINDA  NIPO  TAYARI KATIKA JAMBO  KUU MOJA LAKULETA  MABADILIKO  MAKUMBWA KAMA KUSAIDIANA KUFUNGUA BISHARA  NDOGONDOGO, HILI TUWEZE KUTUSAIDIA  MFUKO WETU WA JUMUIYA  KUWEZESHA KILA MTANZANIA KUWA NA HEALTH INSURANCE  NA LIFE INSURANCE KWA BEI NAFUU KWA JUMUIYA NA TUWEZE  KUFUNGUA DAY CARE KWA WATOTO ZETU WA JUMUIYA YETU  KUWEZA KUISAIDIA TIMU YETU YA MPIRA ,KUSUPPORT WENZETU WENYE BIASHARA ZAO KAMA FASHION NA MITINDO TUWEZE KUFUNGUWA MIGAHAWA  YA CHAKULA KWA SABABU TUNA  WAPISHI WAZURI KWENYE JUMUIYA YETU .NAPIA KUKUTANA  NAKUCHAINGIA MAWAZO  YA KILA MMOJA WETU KWAHIYO BASI HAYA YOTE YANAWEZEKA  KAMA TUTAKUWA NA USHIRIKIANO KWA PAMOJA.


 NDUGU MTANZANIA KWA PAMOJA NAWAOMBA TUBADILIKE TUFUFUE JUMUIYA YETU  YENYE UPENDO NA AMANI .

23 comments:

Anonymous said...

asante kwa taarifa za uchaguzi kura yangu umepata dada je uchaguzi lini na wapi?

Anonymous said...

Tuambie utafanya NINI? wewe unataka Kura tu. Mbona mwenzio Bwana Sandaly Kajieleza Mara mbili. Wewe Vipi? Tupesera zako na Historia yako.
Mdau DMV

Anonymous said...

we Mdau wa pili ...hapo siunaona dada yetu kashajieleza sera zake..au kwa vile sandaly alijieleza mara mbili na yeye ni lazima kwani kujieleza mara mbili,kila mmoja ana style yake,Mdau wa pili jaribu kujenga bali sio kubomoa kwa kuanza kutafuta weakeness za dada Loveness.
mimi kura yangu unayo kwasababu umeonesha ni dada unayejituma na unataka mabadiliko.
Mdau-Kapuni.

Anonymous said...

Kura yangu umepata my sister, tunataka changes DMV na changes zitaanza endapo Watanzania wenzangu mtamchagua Loveness! Tujumuike pamoja jumapili kumchangue Loveness kwa Maendeleo yako na jumuia yako DMV!

Anonymous said...

na hizo biashara ziwe kwa manufaa ya watanzania wa DMV na siyo personal interest

Anonymous said...

Fashion show? Wapishi wazuri? Comeon we deserve better?

Anonymous said...

sera zako ni nzuri tu ila utekelezaji wake unahitaji nguvu za ziada na umakini,lakini hilo litawezekana tukiwa na umoja na ushirikiano na upendo.
jamani nasikitika sana watanzania tunapoleta mambo ya ccm,chadema ,uislamu ,ukristo nk. tujaribu kuachana na hayo mambo kwani dunia nzima tunajulikana kwa kuwa kitu kimoja bila udini,ukabila,wala ubaguzi wa aina yoyote,hilo muhimu sana.
nina swali,dada Loveness elimu ni muhimu sana kwa watanzania ,utasaidia vp ktk hilo,hasa tuliopo hapa,jamni tunaumia acheni. na mwisho wa siku elimu yetu ni faida kwa taifa letu kwa ujumla na sio personally only.
bi mkora DC

Anonymous said...

Daycare usinge itaja hapa umesahau ule ugomvi? Ulivomchamba binti wa watu? Upati kura yangu

Anonymous said...

Lue unapendelea. Kwanini huwapi wagombea wengine video airtime? Kuna mgombea yeyote mwenye uongozi katika chama chochote cha kisiasa inabidi ajiuzulu kwanza. Tunaomba wagombea msisitize life insurance maana misiba inatukumba sana na mtu usipochangia unaonekana mbaya hata kama huna kazi.

Kenge said...

Unafki pembeni, mimi sikupi kura yangu. Sidhani kama kuna mtu ambae hafahamu sababu za jumuiya zilizopita kuvunjika. Watanzania tusipigiane kura kwa kujuana ama ushabiki, tuangalieni mawazo ya hawa watu yatatusaidia vipi. La sivyo tutajikuta tunarudi kule kule tulikotoka. Angalau bwana Iddi nilikuwa simfahamu lakini kupitia historia yake ya uongozi na jumuiya alizopitia AM CONVINCED kwamba kazi ataiweza. Sasa dada ulishawahi kuwa katika jumuiya yoyote ? Ulishiriki vipi katika hiyo jumuiya? Kuna maswali so basic ambayo unaweza ukatufanya tukuamini lakini hujafanya hivyo. Tuondokaneni na masuala ya kusema nampigia fulani kura kwa sababu ni mwanamme mwenzangu, ama ni mwanamke mwenzangu au ni wa dini yangu. Hya mambo hayatotufikisha kokote.

Wadau wengine hapo juu wanadai wanataka changes na changes zitatokea iwapo loveness atachaguliwa, HOW? Kuongea na kutenda ni vitu viwili tofauti, na kama mtu hana historia ya uongozi na kumpigia kura is a bet am not willing to take, i've learned through history of the past community.

Am sure kuna wengi ambao ni "bendera hufuata upepo", hawa ndio watakaosaidia kubomoa hii jumuiya maana wanapiga kura kwa kujuana, ushabiki maandazi, na sababu uchwara na si kutokana na mawazo yao.

Pls pls mpwa naomba usibanie hii comment, haijatukana wala kukiuka chochote katika uandishi.

Anonymous said...

Wagombea tunaomba mpunguze michango. Tumechoka, uchumi siyo mzuri. Kama mtu hana makaratasi anahangaika sana kupata kazi sasahivi. Sasa mkitushindilia amichango ya kila siku bila kujali hali ya uchumi iko vipi, mtakuwa mnatuonea na matokeo yake watu wataamua kujitenga. Mnayo kazi kubwa kubwa, hata hivyo ya kurudusha "Trust"

Kenge said...

Na kwa wale ambao wanapanga kutoka out of state (MAJESHI) kuja kupiga kura huku tafadhali msijisumbue maana mtaaibika.

Anonymous said...

DMV DADA LOVENESS KWA AMBAE ANAMJUWA VIZURI ANAUPENDO TUWEKE NYUMA KILA MTU ANA MABAYA YAKE KAMA BINADAMU AMESAIDIA HII JAMII YETU SANA SIO MISIBA PEKE YAKE WALA HARUSI NI NANI HAMFAHAMU?LABDA CHUKI BINAFSI ZA BINADAMU MIMI NADHANI TUKIMCHAGUA AKAWA NA BODI NZURI ATAFANYA VIZURI NA SIO BODI PEKEE KWA WOTE WANA DMV ANAMOYO MZURI SANA WA KUJITOLEA HALINA UBISHI KABISA TUMUUNGE MKONO MBONA SIJAONA WATU MKIOMBA KAMA YEYE WANAWAKE WA DMV MYAYUE MWEZENU MSILETE AIBU MWANAMKE MWENZENU LOOH!!

Anonymous said...

KWANNZA HONGERA MAMA SIO MCHEZO NAJUWA WATACHONGA LAKINI YOU DESARVE THIS SAMAHANI PEOPLE DMV MSIPINGE PLEASEEEE!! HATER SASA MTULIE KIDOGO

Anonymous said...

wewe hapo juu umesoma vizuri kweli ?hapo alipo andika siameisha jielezea huyo aliyejielezea mara mbili si yeye .Love achana nao hao unajua Washington Dc ni jalala kwa hiyo mengi tu yatasemwa ziba maskio songa mbele wa kukatisha tamaa wapo kwani usipopata huo urais ndiyo mwisho wako?achana nao hao ili mradi umeonesha You can

Anonymous said...

hivi wewe dada unadhani wa tanzania ndo wale wa kijijini maana unaongea kama unaomba kura kijijini lol hivi hujui watanzania wapo wene maendeleo makubwa ambayo hujaaeleza hapo nakwanza suala la elimu hujalitaja kabisa mbona sikuelewi inabidi uhamasishe watu waende shule ili wakija tudi kwao wawe ni watu waloelimika na kuhusu hizo biashara je mtu kama hata papers za uhamiaji itawezekana?

Anonymous said...

Wadau DMV tuache utani- Kwa interview ya Iddi Sandaly na maelezo ya Loveness- Iddi kafunika bovu. Tuacheni utani Iddi yupo more organised na maelezo yake yanaonyesha he is smart, fair and reliable leader.

Anonymous said...

Nyerere angekiwepo angelia machozi. Karne ya 21 tunazungumzia udini? We need to grow up guys. Nafasi ya kugombea urais ipo kwa kila mwana DMV. Kwanini sisi tunaolaumu hamtukuchukua forms isipokuwa ni Iddi na Loveness pekee? Tunaogopa nnini? Hawa wawili ni mashujaa jamani. Tutapata muda wa kuwauliza maswali hiyo Jumapili, na wao watatoa majibu. Halafu tutaamua kila mtu atachagua jinsi anavyopenda. Tupendani watanzania. Tupo ugenini jamani. Tusimpende na kumchangia pesa mtanzania mwenzetu baada ya kifo jamani. Maisha yenyewe haya tunayoishi ni mafupi sana ndugu zangu. Kwani urais wa jumuiya ya watanzania ni kitu cha ajabu sana? Tusipopendana sisi kwa sisi hata hiyo jumuiya itatushinda kama hapo nyuma. Tupendane, tuheshimiane na tuwe kitu kimoja wandugu.

Anonymous said...

TUMEPATA TAARIFA YA KUWA JANA UMEMUHOJI LOVENESS MBONA HUJAIWEKA HIYO INTERVIEW YAKE AU NDO UMENYIMWA NA UBALOZI KUWEKA ACHA USHAMBA KABISA HAPA HATUTAKI UPENDELEO MAANAKE HII BLOG INAJULIKANIKA KWA UPENDELEO NONSENSE WEKA HIYO INTERVIEW YA HUYO MWANAMKE.

Anonymous said...

luka sio vizuri mbona vitu vya loveness hauweki jamani ?tumetuma comment zetu nzuri unazibania

Anonymous said...

kuna uwezekano Iddi na loveness wakawa wote viongozi,mmoja president mmoja msaidizi.please tufikirie hilo kama litawezekana.pia tumple kipindi kifupi cha mwanzo yeyote atakae chaguliwa ili akiboronga tumtoe mapemaaaa!!pia jumuiya iwe na website watu tutoe maoni.

Anonymous said...

hivi wewe Loveness unafikiri uongozi ni kitu rahisi? sio hivyo, uongozi unahitaji mambo mengi sio lelemama kwa kweli mimi kura yangu hupati

Anonymous said...

NASIKITISHWA SANA NA UPUUZI HASWA NA BAADHI YA WANAWAKE WA DMV.KAMA MNACHUKI BINAFSI HAPA SI MAHALA PAKE KUNA RECREATIONAL PARKS NA WALL ZENU ZA FACEBOOK.UPUMBAVU WENU WAKUGOMBANIA MADEREVA MSITULEETEE HAPA.TUNATAKA JUMUHIYA YENYE AMANI NA MAENDELEO YA VIZAZI VYETU(WATOTO WETU) KWANI HAPA NDO TUNASHI(U.S.A), HATUISHI TANZANIA.
NAMKIENDELEA NA KUCHEZA NGOMA MNAYOICHEZA TUTAWATENGA KATIKA JUMUHIYA ILI MUANZISHE JUMUHIYA YENU YA UMBEYA , MAJUNGU,MASENGENYO,NA ROHO MBAYA.WENGI WENU MSHAKUWA, MNAITWA MAMA(MNAWATOTO)SIJUI NI MFANO GANI MNAONYESHA.
PIA NADHANI MNA- BIPOLAR ,DEPRESSION NA FRUSTRATION ZA MAISHA.(SEEK FOR HELP)

WE DESERVE BETTER!