Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amembeba mtoto Anna Julia Telles mwenye umri wa miezi mitatu anayepata matibabu ya kansa katika Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa huo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili. Hospitali hiyo inatoa dawa aina ya chemotherapy kwa wagonjwa ambao ni watoto na inatibu asilimia sabini ya kansa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimtazama mtoto anayepata matibabu ya kansa katika Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa huo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili. Hospitali hiyo ambayo inapokea wagonjwa 4000 kwa mwezi inatibu asilimia sabini ya kansa na hivyo kuwawezesha wagonjwa ambao ni watoto kuendelea kuishi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiangalia moja ya bidhaa zinazouzwa na Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa wa kansa kwa ajili ya kupata fedha za kuwasaidia watoto hao huku Afisa Ubalozi wa Tanzania nchini Brazili Tabu Makata akimuangalia. Hospitali hiyo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili inatoa dawa aina ya chemotherapy kwa wagonjwa ambao ni watoto na inatibu asilimia sabini ya kansa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsikiliza mfanyakazi wa Hospitali ya watoto waougua ugonjwa wa kansa akielezea jinsi hospitali hiyo pamoja na jamii inavyotoa huduma ya kujitolea kwa wagonjwa. Hospitali hiyo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili inatoa dawa aina ya chemotherapy kwa wagonjwa ambao ni watoto na inatibu asilimia sabini ya kansa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa Hospitali ya watoto wanaougua ugonjwa wa kansa Marli Aparecide dos Santos mara baada ya kumaliza ziara yake ya kutembelea hospitali hiyo iliyopo mjini Brasilia nchini Brazili. Hospitali hiyo inatibu asilimia sabini ya kansa na hivyo kuwawezesha wagonjwa ambao ni watoto kuendelea kuishi.
Picha na Anna Nkinda - Maelezo.
No comments:
Post a Comment