Bw. Yacob Kinyemi
Ndugu watanzania wenzangu,Kwanza kabisa natoa shukurani zangu za dhati kwa kunipa nafasi ya kugombea nafasi za uongozi katika Jumuiya yetu ya watanzania katika nafasi ya katibu wa jumuiya. Najua nisingeweza kufika katika hatua ya uchaguzi kama sio ushirikiano wenu mlio uonyesha wa hali na mali. Shukurani za pekee ni kwa watanzania wote mlioweza kufika siku ya tarehe ya uchaguzi kwani ulikuwa wa kihistoria na mliweza kuacha shughuli zenu na kujumuika kwa pamoja.
Kama mnavyojua uchaguzi umekwisha na tumeweza kuwachagua viongozi wetu hawa imara katika kutuongoza katika jumuiya hii teule. Vile vile tukumbuke, tumewachagua viongozi wetu hodari si kwa misingi ya dini, siasa au kabila, bali tumewachagua kwa sabu ya Utanzania wao na katiba ndio itakuwa dira ya uongozi wao. Natao pongezi kwa Rais Iddy sandaly na Katibu Amos cherahani kwa ushindi wao huo. Hivyo basi mimi na nyinyi tutoe ushirikiano wetu wa hali na mali katika kipindi hichi cha uongozi wao. Na mimi nanaamini tumepata timu yenye viongozi madhubuti itakayoweza kuleta maendeleo katika jamii yetu (DMV). Basi, katika kipindi chote hicho cha kampeni za uchaguzi kama kuna mtanzania yoyote niliweza kumkosea ninaomba msamaa. Na mimi nimeshakwisha msamehe kila aliyenikosea.
Hivyo basi uchaguzi umekwisha na sasa tuwasaidie viongozi wetu mawazo yatakayoweza kuleta maendeleo katika jumuiya yetu. Tukumbuke mafanikio ya jumuiya yetu yataletwa na sisi watanzania kwa kusaidiana na viongozi wetu.
Mwisho, mungu wajalie viongozi wetu katika kazi hii ngumu ya kujenga jumuiya yetu ya watanzania (DMV) ambayo ni changa.
Asanteni watanzania wenzangu,
Mungu ibarik Tanzania,
Mungu ibariki Afrika
No comments:
Post a Comment