Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, imefichua ufisadi wa kutisha katika Wizara ya Maliasili na Utalii, kwa kutoa vibali vya uwindaji kwa kampuni hewa na kuruhusu usafirishaji wanyama hai na kupendekeza Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, awajibishwe.
Mbali na Maige, kamati pia imependekeza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Ladislaus Komba, naye awajibishwe kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa ndani ya wizara hiyo. Dk. Komba kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Uganda.
Kamati hiyo ilichunguza utaratibu uliotumika katika kukamata na kuwasafirisha twiga nje ya nchi na utaratibu uliotumika kugawa vitalu vya uwindaji wa kitalii kwa msimu wa 2013 na 2018.
Akitoa taarifa ya kamati hiyo bungeni jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, James Lembeli, alisema wamebaini udanganyifu mkubwa katika ugawaji wa vitalu na utoaji wa vibali kwa kampuni.
Lembeli alisema kampuni ya Jungle International ingawa ilipewa vibali vya uwindaji na wizara, lakini siyo kampuni halali ya kuendesha biashara ya wanyamapori.
Alisema taarifa za Mamlaka ya Usajili wa Kampuni (Brela) zimethibitisha kuwa kampuni ya Jungle tangu Desemba 28, mwaka 2001 ilishabadili jina la Jungle Auctioneers and Brokers Company ambayo inafanya shughuli za udalali.
Alisema ingawa kampuni hiyo tangu mwaka 2001 ilibadili jina na kazi, lakini hadi Desemba 2011 imeendelea kushiriki shughuli za wizara kwa jina lisilokuwepo.
Lembeli alisema walibaini kuwa kuna kampuni nyingi zilipewa vibali vya uwindaji bila hata zenyewe kuomba shughuli hiyo kwa maandishi, hali inayoashiria kuwa kulikuwa na mazungumzo baina ya wahusika kabla ya kutolewa vibali hivyo.
Alisema kibali kilichotolewa kwa kampuni ya Jungle kumakata wanyama kiliandaliwa makusudi kwa lengo la kutoa mianya ambayo itasababisha rasiliamli za taifa kutumika kwa njia isiyofaa.
Lembeli alisema kampuni kama Mwanauta, Saidi Kawawa na Malagarasi zilipewa vitalu tena vya daraja la kwanza na pili wakati kamati ya kumshauri waziri kuhusu ugawaji wa vitalu ilimshauri asizipatie kampuni hizo vitalu.
Alisema uchunguzi wa kamati ulibaini kuwa kibali alichopewa kampuni ya Jungle International kilielekeza ukamataji wanyama kufanyika katika wilaya tatu ambazo ni Longido, Simanjiro na Monduli.
Alisema jambo hilo ni kinyume cha kanuni kwani kibali cha kukamata wanyama ni lazima kiainishe wilaya moja na endapo kutakuwa na ulazima wa kukamata katika zaidi ya wilaya moja, basi vitolewe tofauti kwa kila wilaya.
“Mheshimiwa Spika vibali vya aina hii vinachochea udanganyifu kwa mfanyabiashara kuweza kuwinda wanyama hao katika sehemu zote na kujipatia wanyama wengi zaidi ya aliopewa na kwamba vibali vingi vilivyotolewa na Idara ya Wanyamapori vimeandikwa kwa mtindo huo,” alisema.
Alisema kutokana na hali hiyo, kamati hiyo ilipendekeza kwamba Bunge liitake serikali kukomesha udanganyifu wa aina hiyo na wote wanaohusika wachukuliwe hatua za kinidhamu.
Alisema kwa kuwa serikali iliipa kibali kampuni ya Jungle ambayo wala haikuomba inaonyesha kuwa kuna harufu ya rushwa na uhujumu uchumi.
Lembeli alisema Bunge liitake serikali kutoa maelezo ya kina ni kwa nini kibali kilitolewa kwa kampuni isiyo halali na kuipatia wanyama ambao haikuomba na wahusika wote wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Lembeli alisema kuwa uchunguzi umebaini kuwa Kamran Ahmed raia wa Pakistan ambaye mwaka 2009 alijitambulisha kwenye Idara ya Wanyamapori kama mwakilishi wa serikali ya Jiji la Karachi na akaingia mkataba na aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori , Erasmus Tarimo, kwa niaba aya serikali na kusababisha tembo wanne kusafirishwa nje ya nchi kinyume cha sheria.
Alisema kwa ushahidi uliopo katika kikosi cha ujangili Arusha, Kamran aliwahi kuwa na kesi nyingi za kujihusisha na ukamataji na usafirishaji wa wanyamapori kinyume cha sheria.
Alisema ingawa kwa mujibu wa sheria za wanyamapori 2009, hairuhusiwi kutoa ama kumiliki kadi ya ukamataji wanyamapori kwa raia wa kigeni, lakini inashangaza kuona Kamrani ana kadi namba 0016929.
Lembeli alisema kamati yake imependekeza kwa Bunge liitake serikali ichukue hatua kali za kisheria dhidi ya aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Wanyamapori, Erasmus Tarimo na Kamran Ahmed anayemiliki kibali hicho pamoja na watumishi wengine waliohusika katika sakata hilo.
MAWAZIRI WAGANG’ANIWA
Wakati huo huo, wabunge wameendelea kuwashinikiza mawaziri waliopwaya kwenye nafasi zao kung’oka kwa hiyari yao na kwamba wakigoma kufanya hivyo wataondolewa kwa kimbunga cha nguvu za wananchi.
SUGU HIKI NI KIMBUNGA
Akichangia ripoti ya kamati ya Bunge ya Maliasili na Utalii bungeni jana, Mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi, alisema mawaziri wasijidanganye kuwa yanayosemwa na wabunge kuhusu kuzembea kwao ni upepo tu na utapita.
“Nasikia kuna mkubwa kawaambia kuwa msijiuzulu haya yanayotokea bungeni ni upepo tu utapita, nawahakikishia huu si upepo ni kimbunga na kimbunga kikipita hata kisipong’oa nyumba kitang’oa bati na bati ni Waziri Mkuu,” alisema.
Mbilinyi alisema hali iliyosababisha Waziri Mkuu aliyekuwa bungeni wakati huo kuangua kicheko.
Mbunge huyo alikuwa akielezea namna alivyokerwa na watendaji wa serikali waliosafirisha wanyama hai kama twiga na tembo kwenda nje ya nchi wakati vyombo vya ulinzi na usalama vikiwepo.
“Twiga ni mrefu kuliko ndege, sasa sijui walimsafirishaje, sijui waling’oa viti vyote vya ndege au vipi, huu ufisadi unaofanywa mheshimiwa Spika utakuja siku moja kusababisha watu tung’oe viti humu ndani kwa hasira ,” alisema.
Alisema sekta ya utalii imeshindwa kuliingizia taifa kipato kikubwa kutokana na usimamizi mbovu wa baadhi ya watendaji serikalini ambao hufanya kazi kwa kuzingatia maslahi yao.
MSIGWA: TSUNAMI INAKUJA
Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Peter Msigwa naye alishindilia msumari kuwa mawaziri ambao watakaidi kung’oka kwenye nafasi zao watakumbwa na tsunami.
Aliwataka wabunge watembelee maeneo ya vitalu waone madudu yanayofanywa na watumishi wa serikali wakiwemo hao wanaosema kuwa kamwe hawajiuzulu.
“Mtu yuko ofisini, lakini hakuna chochote anachofanya kwa maslahi ya nchi, rasilimali za nchi zinatoroshwa kila siku watu wamekaa na kubweteka tu maofisini, nyinyi mnastahili kuachia ngazi, wananchi wamekasirika sana na utendaji mbovu wa mawaziri, ondokeni msisubiri tsunami,” alisema Msigwa.
“Mwekezaji ananyanyasa vijana wetu wa Uhamiaji Kilimanjaro, unakuta mwekezaji kaja kisha analazimisha vijana wetu kwenda kugonga vibali vyao ndani ya ndege zao…hii hata katika sheria za kimataifa haipo, ni unyanyasaji wa hali ya juu,” alisisitiza.
Alisema kuna mwekezaji anayeitwa Amran ambaye anaendesha shughuli za uwindaji kihuni, lakini cha kushangaza hata viongozi wa serikali wanamwogopa na hawawezi kuthubutu hata kufika nyumbani kwake.
MREMA: HUU NI UJAMBAZI
Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustine Mrema, alisema yanayofanyika ndani ya wizara hiyo ni zaidi ya ujambazi kwani mwaka 2010 pekee twiga wawili, tembo na viboko walisafirishwa nje ya nchi kinyume cha taratibu.
Alisema mara kadhaa wabunge wanapowakosoa mawaziri wanaona kana kwamba wanawasakama bure wakati madudu waliyofanya yako wazi na kuna uthibitisho.
“Spika leo tufunge milango asitoke mtu humu hadi kieleweke, haiwezekani watu wakafanya madudu haya halafu wanakuwa na kiburi kuwa hawang’oki, hivi kwa madudu haya mtawaeleza nini Watanzania wawaelewe kwamba mnataka kuendelea na nafasi zenu?” alihoji Mrema.
“Mnaogopa nini kuwajibika wakati mmeshindwa kazi, mnataka wabunge tukae kimya wakati nchi ikiendelea kutafunwa, mbona mimi wakati ule Chavda alipofanya ujanja ujanja akachukua fedha za umma nikiwa Waziri wa Mambo ya Ndani niliwajibika?”
Alisema inashangaza kuona Wizara inampa kibali cha kuwinda kisicho na ukomo rais wa Pakistani ambaye hata hivyo hakuna uthibitisho wowote kwamba anapelekewa wanyama hao Pakistani.
Alisema huo ni wizi wa mchana na kwamba viongozi wa serikali wanaiaibisha serikali kwa kushindwa kusimamia rasilimali za nchi na kutoa vibali kiholela.
“Mtu akiiba kuku anafungwa na wakati mwingine kupigwa, hawa wanaoiba tembo, twiga wanadunda tu, madalali wanalipia vitalu Dola 100,000 wenyewe wanaviuza kwa Dola 600,000 tunaipeleka wapi nchi hii, kampuni hewa zimepewa vitalu kiujanja ujanja, hawa mheshimiwa Spika naomba wapokonywe hivi vitalu,” alisema.
“Mmeshiba sana ndugu zangu sasa semeni inatosha,” alihitimisha Mrema.
HEWA: TUUNGANE
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Maria Hewa, alisema huu ni wakati wa wabunge wote kuungana na kusaidia kuijenga nchi kwa kukosoa uozo unaotendeka.
Alisema mawaziri wanaoshambuliwa wasione kwamba kuna mtu mwenye chuki na nia mbaya dhidi yao, ila watambue kuwa wabunge wana nia njema ya kuiendeleza nchi yao.
“Spika tumetoka mbali na taifa letu naomba tusilibomoe, wabunge wote tuungane kuijenga nchi yetu, tusiogope kukosoana maana nchi hii tumeitoa mbali sana,” alisema.
Mbunge wa Busega, Dk. Charles Tizeba (CCM), alisema vitalu vyote 16 vilivyomilikishwa kwa wawekezaji bila utaratibu unaoeleweka virejeshwe serikalini haraka.
Alishauri iundwe kamati maalum kwa ajili ya kuchunguza fedha zilizotolewa na serikali kwa ajili ya kuwafidia wakulima wakati wa mtikisiko uchumi duniani.
WENJE: TUNATA UWAJIBIKAJI
Mbunge wa Nyamagana (Chadema), Ezekia Wenje, alisema nchi inakumbwa na kashfa mbalimbali kila uchao na kutolea mfano wa Richmond, Dowans, rada na utoroshaji wa wanyama hai na kwamba umefika wakati wenye dhamana wawajibike.
Wenje pia aliishutumu Idara ya Usalama wa Taifa kwa kufanya kazi ya kulinda maslahi ya kisiasa badala ya maslahi ya uchumi.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment