ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, June 27, 2012

Dereva taxi na dereva wa daladala wazichapa kavukavu mchana kweupe




Hujawahi kuudhiwa na ujinga wa dereva wa daladala njiani kiasi cha kukufanya utamani upark gari, umfuate na umtandike vibao? Kwakuwa ni njiani na huwezi kufanya hivyo unaamua kupotezea tu japo hasira zimekujaa.

Lakini hivi karibuni huko nchini Kenya ilikuwa tofauti. Kwasababu ambayo haikujulikana mapema, nini walichoudhiana jamaa hawa, ilibidi dereva taxi na dereva wa ‘Matatu’ wapark gari barabarani kwa utaratibu usio rasmi tena kwenye barabara iliyo busy na kuonesha show ya bure kwa kuzichapa ngumi kavu kavu.


Wakiwa na hasira kama simba dume aliyeshikwa sharubu, jamaa hawa walibadilishana mikono kwa muda mrefu na kuigeuza barabara ya Waiyaki ya mjini Nairobi kuwa show ya WWE.


Iikuwa burudani tu kwa wapiti njia ambao hawakutana kuwaachanisha mafahari hao ili kuwapa nafasi wachapane sawasawa.
Baada ya kuona sasa wameanza kuchoka na kutepeta ndipo mtu mmoja akakimbia kwenda kuwaachanisha jamaa hao ambao mchapano wao uligeuka kama ugomvi wa jogoo usioisha.


Daah! Kazi kweli kweli!
Source: Thesiscrime

No comments: