ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 3, 2012

HOTUBA ZA KUFUNGA SPRITE HASHEEM THABEET CLINIC 2012‏


Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania, Phares Magesa (wa pili kulia), Brand Manager Msaidizi wa Coca Cola, Bi. Warda Kimaro (wa kwanza kushoto), Afisa Utamaduni, Ubalozi wa Marekani, Danna Banks (wa kwanza Kulia), na Hasheem Thabeet (wa pili kushoto) wakati wa kufunga Clinic ya Sprite Hasheem Thabeet 2012 jana jijini Dar.
Naibu Waziri wa Elimu, Mhe. Phillipo Mulugo akisoma hotuba yake wakati wa kufunga Clinic ya Sprite Hasheem Thabeet 2012.
Baadhi ya Vijana walioshiriki Clinic hiyo.
---

HOTUBA YA KUFUNGA CLINIC YA SPRITE HASHEEM THABEET 2012
Mkurugenzi wa Michezo
Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa kikapu Tanzania Ndugu Phares Magesa
Afisa Utamaduni, Ubalozi wa Marekani, Danna Banks
Brand Manager msaidizi wa Coca Cola Bibi Warda Kimaro
Hasheem Thabeet ,
Viongozi wa TBF,
Makocha, 
Wachezaji
wadau wote wa michezo.
Kwa niaba ya Serikali na kwa niaba yangu binafsi napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru TBF kwa kazi kubwa walioifanya ya kuakikisha mafunzo haya yanafanyika katika kiwango kizuri , zaidi napenda kuwashukuru Coca cola kupitia kinywaji cha Sprite kwa kuendelea kufadhili mchezo wa Mpira wa kikapu hasa katika ngazi ya Vijana wadogo, pia nawashukru sana watu wa Marekani kupitia Ubalozi wao hapa Dar Es Salaam kwa kusaidia kuendeleza vijana wetu kupitia mchezo wa kikapu.

Kipekee na penda kumpongeza Hasheem Thabeet kwa kuonyesha thamani yake katika mchezo wa Mpira wa Kikapu na kukubali kutumia muda wake kwa ajili ya Vijana wadogo kuwapa mafunzo na kuinua ari kwa vijana wetu  ili nao wapate kuwa na ndoto na kufika pale alipo yeye.
Nimatumaini yangu mafunzo haya mmeyapokea vizuri mtayazingatia na mtakapo rudi kwenye shule zenu nanyi mkawe mabalozi wazuri na walimu kwa wenzenu ambao hawakupata nafasi kama hii mliyoipata
Mikoa iliyoshiriki kliniki hii ya mwaka huu ni Mwanza, Tanga, Dodoma,Kilimanjaro, Arusha, Unguja, Pemba na mkoa mwenyeji wa Dar es Saalaam hivyo basi ni matumaini yangu mwakani mikoa yote ya Tanzania bara na visiwani itashiriki, naomba wafadhili wajitokeze zaidi kuunga mkono jitihada za Cocacola na Hasheem Thabeet ili tuibue vipaji vingi zaidi katika kikapu.
Ndugu zangu serikali ipo pamoja nanyi katika michezo  kama mnavyofahamu wote kuwa mashindano ya Umiseta na umitashumta yamerudishwa rasmi mashuleni,  hivyo mafunzo haya waliyopata vijana hawa basi yatasaidia kuwaimarisha kimbinu za kimchezo na ni matumaini yangu mikoa iliyoshiriki hapa itafanya vizuri kwenye mashindano yajayo ya shule za sekondari na msingi.
Serikali itaendelea kushirikiana na vyma vya michezo vyote nchini katika kuhakiksha michezo inaimarika mashuleni ikiwa ni pamoja kupeleka walimu wengi zaidi wakasomee taaluma hii katika vyuo vyetu mbali mbali, ikiwa ni sambamba na kuongeza uwezo wa vyuo vyetu vya ualimu  kufundisha michezo.
Narudia tena wito wangu kuwa michezo ni sehemu muhimu ya kujenga vijana wetu kiafya, kielimu na kimaadili na hata kiuchumi hivyo basi ni jukumu la kila mmoja wetu, wanamichezo, wazazi, walezi na wakuu wa shule zote nchini kuhakisha vijana wanapatiwa fursa ya kushiriki katika michezo.
Nafahamu kuwa changamoto ya miundombinu ya michezo bado ni tatizo kubwa katika nchi yetu, hivyo basi Serikali itafanya kila jitihada kushirikiana na wadau wengine kuhakikisha tatizo hili linashugulikiwa ipasavyo katika ngazi zote.
Maombi yenu kwa serikali ya kuomba mpewe kipaumbele katika ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndani wenye hadhi ya kimataifa kama wezenu wa soka na riadha wanavyofaidika na uwanja mkuu wa Taifa, nimeyachukua na nitayafikisha katika ngazi husika ili yaweze kushugulikiwa.
Nawashukuru sana wadhamini wa mafunzo haya kampuni ya Cocacola kupita SPRITE na Hasheem Thabeet na nitoe wito kwa wanamichezo wengine Tanzania kuiga mfano wa Hasheem Thabeet wa kurudisha fadhila kwa jamii nzima ya watanzania na nia yake njema ya kuona vipaji vingine vinaibuka Tanzania.
Niwatakie heri katika mafunzo mengine kama haya yatakyofanyika Arusha juma lijalo.
Natoa wito tena kwa makampuni mengine yajitokeze kudhamini michezo na hususani mchezo wa kikapu.
Niwatakie Safari njema wale wote watakaosafiri kurudi mikoani na niwashukuru wote kuanzia Walimu wenu,Wazazi kwa kuwapa ushirikiano mzuri katika kuchangia kufanikisha malengo yenu.
Asanteni kwa kunisikiliza na sasa nimeyafunga rasmi mafunzo haya ya SPRITE HASHEEM THABEET CLINIC 2012.
Mhe. Phillipo Mulugo (MB)
Naibu Waziri wa Elimu

 ----
HOTUBA YA KUFUNGA  MAFUNZO YA SPRITE HASHEEM THABEET CLINIC
Mhe. Phillipo Mulugo, Naibu Waziri wa Elimu
Mkurugenzi wa Michezo
Afisa Utamaduni, Ubalozi wa Marekani, Dana Banks
Brand Manager Msaidizi wa Coca Cola Bibi Warda Kimaro
Hasheem Thabeet ,
Viongozi wa TBF,
Makocha, 
Wachezaji
Wadau wote wa michezo.
Kwa niaba ya Wanamichezo wote hususani mchezo wa kikapu  napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru Coca Cola kupitia kinywaji cha Sprite kwa kufadhili mchezo wa Mpira wa kikapu hasa katika ngazi ya Vijana wadogo, pia nawashukru sana watu wa Marekani kupitia Ubalozi wao hapa Dar Es Salaam kwa kusaidia kuendeleza vijana wetu kupitia mchezo wa kikapu.
Namshukuru sana Hasheem Thabeet  kwa kukubali kuendendesha mafunzo haya kwa kujitolea ikiwa ni sehemu ya mchango wake kwa jamii.
Mikoa iliyoshiriki kliniki hii ya mwaka huu ni Mwanza, Tanga, Dodoma,Kilimanjaro, Arusha, Unguja, Pemba na mkoa mwenyeji wa Dar es Saalaam hivyo basi napenda ni matumaini yangu mwakani miko yote ya Tanzania bara na visiwani itashiriki, naomba wafadhili zaidi kujitokeza na kutuunga ili tuibue vipaji vingi zaidi katika kikapu.
Tunaomba Serikali kupitia wizara yako iimarishe mafunzo ya walimu wa michezo kwa kuongeza vyuo vinvyotoa taaluma hiyo, ikiwa ni pamoja kuwadhamini baadhi ya walimu waliopo ambao wanafundisha michezo kwa mazoea tu na si kwa utaalamu, sasa wakasomee taaluma ya michezo.
Nachukua nafasi hii kumshukuru sana Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuthamini michezo na mara kwa mara amekuwa akitusaidia pale ambapo tunahitaji msaada, mwaka jana alitusaidia tukaweza kupeleka timu zote zote mbili za wanawake na wanaume katika mashindano makubwa ya kanda ya tano na ya awali kutafuta bingwa wa kikapu Afrika.
Mhe. Waziri mwaka huu mashindano haya yatafanyika Tanzania, mwezi December, hivyo basi tunaomba utufikishie maombi yatu kwa Mhe. Rais na Serikali nzima ili watuunge mkono kufanikisha mashindano haya.  Bingwa wa mashindano haya atapata nafasi ya kwenda kushindana kutafuta bingwa wa kikapu wa Afrika kwa timu za Taifa.
Tunaomba serikali ifanye marekekebisho ya msingi katika wanja wa ndani wa sasa ili uwe katika hali nzuri zaidi, ikiwa ni pamoja na kuziba sehemu zinazovuja, kurekebisha miundombinu ya maji na vyoo na kutengeneza mfumo wa hewa (ventilation) na kurekebisha majukwaa.
Tunaomba hili lifanyike kwani ni juzi tu tumeshuhudia mchezo wa kimataifa wa netboli ukisimama kuchezwa kutokana na paa kuvuja na kama mvua isingeisha basi mchezo ule usingeendelea, hii ni aibu kwa Taifa. Pia sisi mwaka huu tulikiwa na ugeni wa timu ya AND1 toka USA, mchezo wake wa Mwnza haukufanyika kutokana na mvua kuwa kubwa na hakuna kiwanja cha ndani katika jiji hilo.
Tunaomba marekebisha hayo ya msingi yafanyike kwa uwanja ulipo sasa wakati tunasubiri ahadi ya ujenzi wa awamu ya pili ya uwanja wa Taifa .
Ombi letu kubwa ni kupewa kipaumbele katika ujenzi huo wa uwanja mkubwa wa ndani wenye hadhi ya kimataifa kama wenzetu wa michezo mingine walivyojengewa.
Na pia tunomba utufikishie katika ngazi husika wito wa kutengwa maeneo maalumu kwa ajili ya michezo katika kila kata ili pale atakapopatikana mfadhili basi iwe rahisi kujenga uwanja.
Pia tunaomba kila shule inayopew kibali iwe na sehemu ya kutosha kujenga viwanja vya michezo.
Nakushukuru sana Mhe Waziri kwa kubali kuja kutufungia mafunzo haya na nawashukuru sana wadhamini wa mafunzo haya kampuni ya Cocacola kupita SPRITE na Hasheem Thabeet.
Nichukue nafasi hii kuufahamisha umma kuwa mafunzo mengine kama haya yatafanyika Arusha kwa kusaidiana na watu wa Marekani kupitia ubalozi wao hapa Dar Es Salaam na pia kampuni ya Cocacola, mafunzo hayo yatafanyika tarehe 9 na 10, watu wa Arushe mjitokeze kwa wingi.
Naomba makampuni mengine yajitokeze kudhamini michezo na hususani mchezo wa kikapu.
Niwatakie Safari njema wale wote watakaosafiri kurudi mikoani na niwashukuru wote kwa ushirikiano mzuri katika kuchangia kufanikisha mafunzo haya.
Asanteni kwa kunisikiliza
Phares Magesa
Makamu wa Rais- TBF

No comments: