Kutoka kushoto ni Mwanachama mpya Ndugu Hussein Kauzela, Katibu wa Tawi Ndugu Liberatus Mwang'ombe, Mweyekiti wa Tawi Ndugu Kalley Pandukizi na Katibu mwenezi Ndugu Cosmas Wambura.
Mwenyekiti wa Chadema Washington DC akimkabidhi kadi mwanachama mpya ndugu Hussein Kauzela. Katikati ni Katibu wa Tawi Ndugu Liberatus Mwang'ombe
Mwenykiti wa Tawi akimkabidhi kitabu cha Katiba na Sera za Chadema Ndugu Hussein Kauzela
Pichani ni Kadi na Kitabu cha Katiba na Sera za Chadema.
Wadau wakipongezana katika hafla ya kukabidhi kadi wanachama wapya
Wadau wakiwa mbele ya gari iliyokabidhiwa na mwanachama wao mpya.
Mwenyekiti wa Chadema Washington DC akiwa ameshika funguo za Gari walilokabidhiwa na mwanachama wao mpya Ndugu Kauzela
Pichani Gari aina ya Chevy Suburban walilokabidhiwa Viongozi wa Chadema Tawi la Washington DC na mwanachama mpya ndugu Hussein Kauzela.
Viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA tawi la Washington DC, Marekani jana tarehe 23 JUNE 2012 Wamekabidhiwa gari aina ya Chevy Suburban na Mwanachama wao mpya Ndugu Hussein Kauzela Msabaha. Akiongea katika hafla hiyo Mwenyekiti wa Chadema Washington DC Ndugu Kalley Pandukizi amemshukuru sana mwanachama wao huyo mpya na kusema gari hilo litawasidia katika kueneza Sera za Chama kwa Watanzania Wanaoishi Majimbo mengine ya Marekani. Naye mwanachama huyo mpya amesema amejitolea gari lake hilo litumike kwa kazi za chama kwa Ridhaa yake si kwa kushawishiwa na mtu yeyote kutokana na kukubali Sera za Chadema. Mwenyekiti wa Chadema aliongeza kwa kusema anawaomba Watanzania wote wenye kutaka Mabadiliko waige mfano wa Ndugu Hussein Kauzela kwa kukisaidia Chama kwa hali na mali ili waweze kuzidi kukijenga Chama ambacho Wanachama wake ndio washika Dau wakuu kwenye kukijenga Chama.
No comments:
Post a Comment