ANGALIA LIVE NEWS

Monday, July 9, 2012

SHUKURANI ZA DHATI

kwa niaba ya familia ya Jack Korassa tunapenda kutoa shukurani zetu kwa wale wote waliofika na ambao hawakuweza kufika kutokana na kukosa wakati muafaka japo nia ilikuwepo.

Mshikamano na ushirikiano wenu na upendo wa dhati uliopo miongoni mwetu Watanzania hasa katika kipindi hiki kigumu cha ndugu, jamaa na rafiki yetu Jack Korassa kufiwa na Baba yake mzazi kusema ukweli Jack ameguswa sana na kufarijika kwa jinsi mlivyoacha shughuli zenu muhimu na kufika nyumbani na kanisani na kumitia nguvu na kumpa moyo, kusema ukweli hana cha kuwalipa kitakacholingana na hayo makubwa na mazuri mliofanya kwake na daima yatabaki kwenye kumbukumbu ya masha yake ya kila siku na kuomba tuwe na upendo na mshikamano miongoni mwetu.

Pia Jack anatoa shukurani kwa Kaimu Balozi wa Tanzania Nchini Marekani Mhe. Lilian Munanka kwa maneno mazuri yakumfariji aliyotoa kanisani, shukurani za pekee ziwaendee Frank Mhina na mkewe, Aunty na Uncle kutoka North Carolina bila kuwasahau Catherine Molel kutoka Canada na Jack Mbwile kutoka Michigan.

Tunapenda kutoa shukurani kwa kanisa la The Way Of The Cross Gospel Ministries kuweza kwao kutupatia nafasi ya Ibada ya Mzee Joseph Korassa bila kujali muda wa ziada walioupoteza kwa kukaa na sisi mpaka mwisho.

Tunapenda kuishukuru Jumuiya ya Watanzania DMV kwa ushirikiano wao waliouonyesha kwa mfiwa.

Mwisho tunatoa shukurani kwa marafiki wa Jack kwa ushirikiano, mshikamano na moyo wa upendo mliouonyesha kwake na kuwezesha kufanikisha shughuli za msiba wa Baba yake Mzazi, Mungu awabariki na awazidishie maradufu.

No comments: