ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, August 23, 2012

AMSHA AMSHA YA TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2012 YAZIDI KUWAZINDUA WAKAZI WA MJI WA MOSHI NA VITONGOJI VYAKE‏



Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Dr Msengia  akiaga baada ya kuitembelea timu Serengeti Fiesta 2012 Mkoa wa Kilimanjaro jioni ya leo. Katikati ni Erick Kussaga ambae ni Mzalishaji wa timu ya Fiesta mkoani humo.


Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Mheshimiwa Dr Msengi akiwa na Afisa Uhusiano wa Clouds Entertainment Co. LTD kwa upande wa Viongozi wa Taasisi za Serikali na Vyama vya Siasa Ndugu Simalenga Simon wakati Mkuu huyo wa Wilaya alipoitembelea timu ya amsha amsha ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012 Mkoani Kilimanjaro jioni hii.Tamasha la Serengeti Fiesta 2012 linatarajia kuzinduliwa rasmi kesho katika uwanja wa chuo cha Ushiriki mkoani humo,ambapo msanii nyota kutoka nchini Kenya,CMB Prezoo ataliongoza jahazi la wasanii mbalimbali kutoka hapa nyumbani,katika tamasha hilo kiingilio kimepangwa kuwa ni shilingi 5000 kwa kila kichwa. 


Mmoja wa washabiki wa tamasha la Serengeti Fiesta damu akiwa na fulana yake ya tamasha hilo lililowahi kufanyika mjini moshi lililopachikwa jina la jipanguze kama uonavyo pichani.Wanaharakati anuai wa tamasha la serengeti fiesta 2012 leo wameamsha amsha wakazi wa mji huo katika maeneo mbalimbali ikiwemo Himo,Stendi kuu ya mabasi pamoja na soko la Mbuyuni na kutoa zawadi ya mafuta ya gari/pikipiki na bajaji kutoka kampuni ya Gapco ambayo ni sehemu ya wadhamini wa tamasha hilo,kwa watu kadhaa ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za awali ya tamasha lenyewe.
kwa picha zaidi read more

No comments: