Waziri
wa Uchukuzi Dkt. Harisson Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA-Ndugu Ephrahim Mgawe pamoja na
wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.
Wengine
waliosimamishwa ni Meneja wa Mafuta ya Ndege Kurasini, Meneja wa JET na
Meneja wa Oil Terminal kutokana na tuhuma za kupotea kwa mafuta na
kuidanganya serikali kuhusu mafuta masafi na machafu.
Kutokana
na kuwasimamisha kazi Wakurugenzi hao Dkt. Harisson Mwakyembe amemteua
Injinia Madeni Kipange kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.
Kufuatia
tuhuma hizo zinazofanywa Bandarini Dkt. Mwakyembe ameunda Tume wa ya
watu saba kufanya uchunguzi kwa wiki mbili na kumpelekea taarifa ofisini
kwake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo zikiwemo za wizi.
Pia
ameagiaza kufikia Septemba Mosi mwaka huu malipo yote yafanyike benki
ili kuondoa rushwa na wizi unaofanyika ndani ya Mamlaka hiyo.
Waziri
Mwakyembe anachukua hatua hizo kutokana na wwadao wengi sasa hawaitumii
Bandari ya Dar es salaam kupitisha mizigo yao kutokana na kutokuwa na
imani na watumishi wake hatua inayoifanya serikali kukosa mapato.
Pia
ameagiza kusimamishwa mara moja kwa Kampuni ya Singilimo ambayo
inajihusisha na kazi ya kubeba mafuta machafu na badala yake itafutwe
Kampuni nyingine.
No comments:
Post a Comment