Siku chache baada ya Serikali ya Tanzania kupitia kwa waziri wake wa mambo ya nje Mh. Bernad Membe kuitaka Serikali ya Malawi kuondoa majeshi na kampuni zinazofanya utafiti wa gesi kwenye ziwa Nyasa ukanda wa Tanzania wakidai kuwa ziwa hilo ni la kwao lote wameanza kufanya hivyo na kuondoka taratibu ukanda huo. Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Mbeya Bw. Abbas Kandoro alisema kuwa kwa sasa eneo hilo hali ni shwari kwani
makampuni, ndege na askari wa malawi waliokuwa wakiendesha shughuli zao kwenye eneo la Tanzania wametii amri na kuondoka kwenye eneo hilo hivyo wananchi wasiwe na shaka bali waendelee na kazi zao za kila siku kwenye ziwa hilo, Mbali na Waziri Membe, viongozi wengine waliozungumzia mgogoro huo na
kuitaka Malawi iache uchokozi ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Samuel Sitta na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya
Nje, Ulinzi na Usalama, Edward Lowassa.
2 comments:
mnataka kuwapiga wenzenu na wao hawataki mapigano na nyinyi wao ni wastaarabu nyinyi watanganyika kila leo mmezoea kutumia mabavu basi mtaona mwisho wenu wenzenu watapata hili ziwa KIULAINI SUBIRINI MIMACHO ITAKUTOKENI KODO KODO HAMNA SERA TANZANIA KAZI UTAPELI DUNIA IMESHAMKA KILA NCHI INATAKA CHAKEEE
We ongelea hoja sio UPUUZI WA WATANZANIA. sema itatukea nini na kwa vipi kisheria au vipi. maana bahati mbaya wana RAIS ambaye anaangalia kipengere kimoja tu cha Heligoland Treaty. Kama watanzania sisi ni wapuuzi, poa, kwahiyo inakuhusu nini upuuzi wetu? na wewe RAIS wenu kuruhusu amshoga na wasagaji, nani mpuuzi? ..... hakuna sehemu yoyote katika ANDIKO LOLOTE KWAMBA MALAWI ni mmiliki wa ziwa. TUNACHOTAKA NI MIPAKA sio NANI ANAMILIKI NINI. nyie ndio wajinga wajinga msioelewa hoj. nENDA KAUMUULIZE RAIS WAKO JOYCE BANDA kilichomtuma aombe ruhusu ya JWTZ kutafiti mafuta ni kitu gani? ha haha JARIBUNI MUONE
Post a Comment