Baadhi
ya wadau wamehoji mavazi ya namna hii kwa Asakri Polisi wa Kike kama
yanakidhi matakwa na kuweza kumsitiri Askari wa kike wa Jeshi la Polisi
awapo katika Utekelezaji wa Kazi zake za kila siku kwa kuwahudumia
wananchi.
Pia wadau wanahoji kuwa Waraka wa Utumishi wa Umma na 3 wa mwaka 2007 kuhusu mavazi kwa watumishi wa umma kama unatekelezwa na Jeshi jeshi hilo ama au wahusu.
Aidha
wadau hao wamesema ipo haja kwa Jeshi la Polisi hapa nchini kubadili
mavazi hayo kwa Wanawake na kuamuru zivaliwe surwale wakati wote wawapo
kazini maana wapo askari wa kikle wanaoenda doria na sketi hizo jambo
ambalo ni rahisi kutokea vitendo vya uzalilishaji kwao, na badala yake
wameshauri zivaliwe wakati wa shughuli maalum tu kama vile
sherehe za kijeshi na Kitaifa ambapo hakuihitaji pilika pilika za hapa
na pale ndio wavae Sketi huku pia wakidai sketi hizo ziwe ndefu kiasi
cha kuvuka magati.
Hata
hivyo Sketi fupi mfano wa hiyo iliyovaliwa na Askari hiyo ambaye Blog
hii imemhifadhi haiendani na sheria za mavazi ya Mtumishi wa Umma ambayo
hapaswi kuvaa nguo fupi kwa Mujibu wa waraka wa Utumishi wa Umma.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS
Kumb. Na. EG.45/86/01/”A”/2 12/9/2007
WARAKA WA UTUMISHI WA UMMA NA 3 WA MWAKA
2007 KUHUSU MAVAZI KWA WATUMISHI WA UMMA
Utangulizi:
Waraka
wa Utumishi Na. 1 wa mwaka 1971 unaohusu mavazi ulitokana na mwongozo
uliotolewa na Chama cha TANU kuhusu mavazi. Madhumuni ya waraka huo
ilikuwa kuimarisha heshima ya Taifa kwa kuhakikisha kuwa watumishi wa
Serikali wanavaa mavazi ya heshima wanapowahudumia wananchi. Waraka huo
uliainisha baadhi ya mifano ya mavazi ambayo yalionekana hayafai na yale
yanayofaa kwa wanawake na wanaume, utengenezaji wa nywele unaofaa na
usiofaa na vipodozi visivyokubalika.
Hali ilivyo sasa:
2.
Tangu waraka huo ulipotolewa kumekuwepo na mabadiliko makubwa ya
mitindo ya mavazi, nywele na vipodozi. Mabadiliko ya mitindo ya mavazi
ni jambo lisiloepukika. Hata hivyo baadhi ya mitindo hiyo ya mavazi
inashusha heshima na hadhi ya utumishi wa umma kama itaendelea
kuvaliwa
na ni kinyume na kifungu cha 2 (e) cha kanuni za Maadili ya utendaji
katika utumishi wa umma za mwaka 2005 Hata hivyo kumekuwepo na tatizo la
kutokuwepo na tafsiri inayoeleweka juu ya mavazi gani ni ya heshima au
yanayokubalika na yasiyokubalika mahali pa kazi.
2
Uamuzi wa Serikali:
Tafsiri
ya mavazi ya heshima hutegemea mila na desturi ya jamii husika. Katika
utumishi wa umma mavazi ya heshima kwa mtumishi wa umma ni yale ambayo
yanazingatia mila na desturi za taifa letu ambayo yanapovaliwa
hayaonyeshi sehemu ya maungo ya mwili ambayo hayakuzoeleka kuachwa wazi,
hayabani na ambayo hayana michoro au maandishi ya kudhalilisha wengine
au yanayoonyesha ushabiki wa kitu fulani. Kwa hiyo waraka huu unatoa
ufafanuzi kuhusu mavazi nadhifu yanayopaswa kuvaliwa kazini kwa kutoa
mifano michache ya mavazi ambayo siyo ya heshima na ambayo hayakubaliki
katika utumishi wa umma kwa jinsi zote mbili.
Utekelezaji:
3.
Ufuatao ni ufafanuzi wa mavazi yasiyokubalika mahali pa kazi ambayo pia
yameonyeshwa kwa picha kwenye kiambatisho A na B. Nguo kama “Jeans” na
fulana zinaweza kuvaliwa na watumishi ambao wanalazimika kufanya kazi za
nje ya ofisi.
3.1 Kwa Wanawake
(i) Baadhi ya mavazi yasiyofaa:
• Nguo zinazobana,
• Nguo fupi ambazo zinaacha magoti wazi.
• Nguo ambazo zinaacha sehemu ya mwili wazi kama
vile kitovu na kifua,
• Nguo ambazo zina picha, michoro, na maandishi ambayo hayaendani na shughuli za serikali,
• Kaptura aina yoyote ile kama vile pedo na pensi,
• Nguo zinazoonyesha maungo ya mwili (transparent).
• Suruali za “Jeans”,
• Suruali yoyote iliyoachwa bila kupindwa,
• Fulana – “T-Shirts” (Hizi zivaliwe tu wakati wa shughuli maalum inayotambulika),
•
Nguo ambazo ni za kazi maalum – michezo, kazi za nje au burudani. Hizi
zivaliwe mahususi wakati wa utekelezaji wa shughuli hizo,
• Nguo yenye maandishi ya chama chochote cha siasa au ushabiki wa kitu fulani,
• Nguo yeyote inayopingana na maadili ya utumishi wa umma.
(ii) Nywele zisizofaa:
• Nywele chafu na ambazo hazikutengenezwa vizuri.
(iv) Viatu visivyofaa
• Kandambili,
• Viatu vya michezo (isipokuwa wakati wa shughuli
maalum za michezo),
3.2. Kwa Wanaume
(i) Baadhi ya mavazi yasiyofaa:
• Nguo ambazo ni za kazi maalum kama vile michezo (Hizi zivaliwe wakati wa shughuli hiyo tu).
• Nguo ambazo zina michoro, maandishi na picha ambazo haziendani na shughuli za serikali.
• Nguo zinazobana,
• Kaptura ya aina yoyote.
• Suruali yoyote inayoachwa bila kupindwa.
• Suruali za “Jeans” na Fulana “T-shirts” (Hizi zivaliwe tu wakati wa shughuli maalum inayotambulika).
• Kikoi au msuli
• Nguo zenye maandishi ya chama chochote cha siasa na yenye kuonyesha ushabiki wa kitu fulani.
• Nguo yeyote inayopingana na maadili ya utumishi wa
umma.
(iii) Nywele zisizofaa:
• Nywele chafu na ambazo hazikutengenezwa vizuri.
• Nywele zilizosukwa mitindo ya aina yoyote ile
• Ndevu zisizotunzwa vizuri.
(iv) Viatu visivyofaa:
• Kandambili,
• Viatu vya michezo( Labda wakati wa shughuli maalum
za michezo).
Mwisho:
4.
Kwa waraka huu waajiri wote wanapaswa kuwaelimisha watumishi kuhusu
mavazi yasiyokubalika na kusimamia kikamilifu suala la mavazi kwa
watumishi wa umma .
5. Waraka huu unafuta Waraka wa Utumishi Na.1 wa mwaka 1971 na unaanza kutumika mara moja.
George D. Yambesi
KATIBU MKUU
(MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA)
No comments:
Post a Comment