KIKOSI CHA WASOMI KUHUTUBIA DOCTORS, ENGINEERS, NA WASOMI WENGI
MKUTANO WA CHADEMA READING
LONDON
Ili kufikia malengo yetu ya kuzunguka kwenye Miji mbalimbali ya UK kuhamasisha Watanzania waishio uk kujiunga na Chadema, kueneza kampeni ya m4c na kufungua matawi mengine, Tawi la Chadema London linapenda kuwatangazia Watanzania wote waishio katika Mji wa Reading na maeneo ya jirani kuwa kutakuwa na mkutano mkubwa wa M4C UK utakao fanyika Tarehe 26/08/2012 siku ya Bank holiday.
Dhumuni la mkutano huo ni kuwahamasisha Watanzania waishio UK kujiunga na chama, kushiriki katika harakati za mabadiliko, kusajili wanachama wapya, kuchagua wawakilishi wa muda kutoka mji wa Reading pamoja na kuanzisha mfuko wa kufa na kuzikana kwa manufaa yawatanzania wote.
HEBU JIULIZE UKIFIWA HAPA UK UTAKWENDA WAPI KUSAIDIWA?
Tumekusudia kuanzisha Mfuko wa kufa na kuzikana kwa sababu mpaka hivi sasa Mtanzania akifariki akiwa UK hakuna taasisi wala ofisi yoyote inayotoa msaada. Jukumu ambalo kwa muda mrefu Serikali yetu kupitia ubalozi wamelipuuzia na kushindwa kulishughulikia na kulisimamia.
Mfuko huu utasaidia katika kumsafirisha Marahemu na Mfiwa pamoja na kusaidia kushughulikia matatizo na usumbufu utakaojitokeza baada ya mtu kufariki dunia na kusaidia matatizo mbalimbali yakiwemo majanga ya dharura.
Pia katika mkutano huo wanachama mbalimbali wa CCM walio na uchungu na nchi yetu na wanaopenda mabadiliko ya kweli watapewa nafasi ya kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama sehemu moja wapo ya kampeni yetu ya Kuvua Gamba na Kuvaa Gwanda ukiwa Ughaibuni.
Mkutano utafanyika siku ya Tarehe 26/08/2012 kuanzia saa saba mchana mpaka saa kumi na mbili jioni, siku ya Bank Holiday. .Risc Reading International Solidarity Centre, 35-39 London Street, Reading, RG1 4PS .
Watanzania wote na wadau mbali mbali mnakaribishwa
SISI SOTE NI NDUGU, TATIZO NI CCM
ni wakati wa kusimama na kusema tumechoka
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA HAWA WAFUATAO
MWENYEKITI: Chris Lukosi 07903828119
KATIBU MWENEZI: Chris Chagula 07405889880
Au tutumie email kupitia chademauk@gmail.com
BAADHI YA WATOA MADA MBALI MBALI WATAKAONGEA SIKU HIYO NI;
DR, LUSINGU
DR, ALEX
ASERI KATANGA (Chairman computers for AFRICA)
Engineer PRUDENCE
LIBERATUS MUSIBA (Msc, Project planning & Management)
NA WENGINE WENGI
HATULALI MPAKA KIELEWEKE!!!!!!!!!!! Peooooople's Power |
1 comment:
londan mfanye kazi please msituaribie chama kama chadema usa wachokifanya ni kutukana na majungu hamna zaidi london people power !!!!
Post a Comment