HARUFU YA KIKWAPA
NDUGU ZANGU WAPENDWA. HARUFU YA KIKWAPA IMEKUA TATIZO KUBWA KWA JAMII YETU NA WATU WENGI WAMEIZOEA HIYO HARUFU KIASI KWAMBA HAWAJITAMBUI KUA WANATOA HARUFU. WATU WENGI WANCHI ZA NJE WAKIJA TANZANIA WANALALAMIKA KUA HARUFU YA KIKWAPA INAWASUMBUA.
HARUFU YA KIKWAPA INATOKANA NA SABABU NYINGI KAMA USAFI WA MWILI, CHAKULA (KAMA RED MEAT). MTU ANAPOTOA JASHO, BACTERIA WANATUMIA NAFASI HIYO KWENDA KWENYE JASHO KUJIPATIA CHAKULA. KADRI BACTERIA WANAVYOKUA WENGI, HARUFU NAYO INAZIDI. KUOGA KUNASABABISHA BACTERIA KUONDOKA HASA KAMA UNATUMIA SABUNI INAYOUA HAO BACTERIA (ANTISEPTIC SOAP). BACTERIA WANAOKAA KWENYE KIKWAPA WANAZIDI PIA KAMA UNATUMIA KITAULO CHA KUOGEA NA KUTOKUKIFUA VIZURI NA KUACHA KISIKAUKE. HIVYO UNASHAURIWA KUKIANIKA NJE KIKAUKE BAADA YA KUOGA, PAMOJA NA TAULO YA KUJIFUTIA ILI VIONDOKANE NA BACTERIA AU KAMA INAWEZEKANA KUFUA KILA SIKU.
KWA SABABU MTU HAWEZI KUSHINDA ANAOGA SIKU NZIMA NI BORA KUTUMIA NJIA ZA KUKINGA HARUFU YA KIKWAPA. NJIA HIZO NI KAMA ZIFUATAZO:
1. KUTUMIA DEODORANTS AU ANTIPERSPIRANTS. DEODORANTS ZINASAIDIA KUONDOA BACTERIA AMBAO WAKO KWENYE KIKWAPA. MARA NYINGI HUA ZINA HARUFU NZURI NA KUNA AMBAZO HAZINA. KAZI YAKE NI KUFANYA BACTERIA WASIKAE KWENYE KIKWAPA. ANTIPERSPIRANTS ZINAZUIA JASHO LISITOKE KWA WINGI. UNAPOENDA KUNUNUA DEODORANT ANGALIA YENYE INGREDIENT INAYOITWA ALUMINIUM CHLOROHYDRATE.
2. KUTUMIA BAKING POWDER. HII NI NJIA RAHISI ZAIDI AMBAYO INATUMIA GHARAMA NDOGO ZAIDI. KUNA PACKET YA BAKING POWDER AMBAYO INAUZWA BEI CHINI YA SHILLING MIA NA ITADUMU KWA MUDA HATA WA MIEZI MITATU. WEKA KIDOGO KWENYE KIGANJA, CHANGANYA NA MAJI HALAFU PAKA KWENYE KIKWAPA BAADA YA KUOGA. HII ITAZUIA HARUFU YA KIKWAPA SIKU NZIMA.
3. VAA NGUO ZA KITAMBAA CHA COTTON AU WOOL. NINA MAANA KWAMBA NGUO AMBAZO NI SYNTHETIC KAPPA POLYESTER AU NYLON ZINAFANYA MTU ATOE JASHO ZAIDI.
4. NYOA NYWELE ZA KIKWAPA. NYWELE ZIKIWA NYINGI ZINAKUA KAMA MTEGO WA BACTERIA NA KUSABABISHA HARUFU.
5. KUNYWA MAJI MENGI. MAJI YANASAIDIA KUTOA SUMU KWENYE MWILI NA KUSABABISHA HARUFU KUPUNGUA.
6. OGA ANGALAU MARA MBILI KWA SIKU NA KUSUGUA VIZURI SEHEMU YA KIKWAPA.
7. VAA NGUO SAFI KILA SIKU.
8. HAKIKISHA HUNA HARUFU Y KIKWAPA KABLA YA KUTUMIA PERFUME KALI. MCHANGANYIKO WA HARUFU YA KIKWAPA NA PERFUME INATOA HARUFU MBAYA ZAIDI.
ASANTE SANA,
RAHELI.
2 comments:
Nashukuru mie mpenzi wangu hata atoke jasho vipi hanuki kikwapa. Na hapki deo wala perfume. Ila kuna watu wanaka vikwapa!
Asante dada Raheli....tumechishwaaa na harufu za vikwapa hasa kwenye mabasi, maofisini, makanisani na Misikitini. Utakuta Msomi mzima ananukaaa hafai na amevaa suti na tai. Halafu kuna wale wanaorudia nguo siku mbili mfululizo. Jamani badilikeniii...mnatia aibuuu...!! Mdau, CA-USA
Post a Comment