Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Ali Mohd Shein, akiwa pamoja na viongozi wakuu wa Zanzibar na viongozi wengine kwenye viwanja vya hoteli ya Bwawani wakati wa sherehe za Baraza la Eid-El- Fitri.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad (kulia) na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Amani Abeid Karume, kila mmoja akiwa na shauku ya kutaka kumweleza mwenzake chochote, walipokutana katika hoteli ya Bwawani kwa ajili ya Baraza la Eid-El-Fitri. Viongozi hawa ndio walioasisi maridhiano ya kisiasa Zanzibar na kupatikana Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na viongozi mbalimbali katika viwanja vya hoteli ya Bwawani walipokutana kwa ajili ya Baraza la Eid-El-Fitri, jana tarehe 19/08/2012.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akibadilishana mawazo na Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohd Shein, kwenye viwanja vya hoteli ya Bwawani walipokutana kwa ajili ya Baraza laEid-El-Fitri, jana tarehe 19/08/2012.
Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
No comments:
Post a Comment