SNOOP Dogg ni miongoni mwa wanamuziki wakongwe ambao wameweza kushikilia hadhi za juu katika chati za muziki.
Hivi karibuni Snoop aliwaacha mashabiki wake vinywa wazi baada ya kutangaza rasmi kuachana na aina hiyo ya muziki na kuhamia kwenye Reggae.
Snoop ambaye anajulikana kupitia nyimbo zake zilizofanya vizuri kama Beautiful, na Drop It Like It's Hot ametangaza uamuzi huo sambamba na jina lake jipya ambapo sasa si snoop dogg bali ataitwa Snoop Lion.
Akitangaza hatua hiyo mbele ya waandishi wa habari nchini Jamaica Snoop, anasema ziara yake nchini humo ndiyo imemfanya kufikia maamuzi hayo baada ya kuhisi amezaliwa upya kwani sasa anataka kufanya muziki ambao utasikilizwa na watu wa kila rika.
Anasema kwa sasa ameamua kujikita katika muziki huo kwa sababu ya kuvutiwa na imani ya rasta na amechukua nafasi ya muhasisi wa reggae duniani hayati Bob Marley anaamini kwamba anakila chembechembe za msanii huyo na hataki kabisa kuja kuacha tamaduni hiyo ya kirastafari.
“Siku zote nimekuwa nikitembea na roho ya Bob Marley na kwa sasa nimeingia rasmi kwenye reggae kuchukua nafasi yake kuuendeleze muziki huu nahitaji siku moja hata nikifa nikumbukwe kama ‘jah’,”anasema Snoop.
Anasema kwa muda wa siku 35 alizokuwepo nchini Jamaica amejikuta akijisikia kuhamia kwenye muziki ambao utasikilizwa na kila mtu katika familia yake tofauti na ilivyokuwa hapo awali akiimba rap.
Anaongeza kuwa ameamua kupumzika kuimba hip hop kwa kuwa amechoshwa na aina hiyo ya muziki pia hakuna changamoto anayokutana nayo kwa kuwa anaumudu vyema na hakuna wa kusumbua kichwa chake katika eneo hilo.
Snoop Lion ameshatambulisha albamu yake ya kwanza katika miondoko hiyo itakayoitwa ‘Reincarneted fall in the fall’ ambayo itafuatiwa na jarida litakalojulikana kwa jina hilohilo.
Snoop Lion ameshatambulisha albamu yake ya kwanza katika miondoko hiyo itakayoitwa ‘Reincarneted fall in the fall’ ambayo itafuatiwa na jarida litakalojulikana kwa jina hilohilo.
Snoop Dogg ni nani?
Msanii huyu ambaye jina lake halisi ni Calvin Broadus alizaliwa Oktoba 20, 1971 karibu na fukwe za mji wa California. Alipata jina la utani la "Snoop" kutoka kwa mama yake kwa kuwa alikuwa alimfananisha mtoto wake huyo na muigizaji mmoja wa kipindi cha katuni.
Msanii huyu ambaye jina lake halisi ni Calvin Broadus alizaliwa Oktoba 20, 1971 karibu na fukwe za mji wa California. Alipata jina la utani la "Snoop" kutoka kwa mama yake kwa kuwa alikuwa alimfananisha mtoto wake huyo na muigizaji mmoja wa kipindi cha katuni.
Baada ya kuhitimu elimu ya sekondari Snoop alikamatwa na polisi zaidi ya mara moja kutokana na kujihusisha na dawa za kulevya ambapo alijikuta akitupwa gerezani mara kadhaa.
Alifanikiwa kukutana na rapa maarufu Dr. Dre ambaye alimuingiza kwenye muziki na kufanikiwa kutopa albamu yake ya kwanza mwaka 1993 iliyoitwa Doggystyle ambayo ilifanya vizuri katika chati za muziki nchini Marekani.
Msanii huyu ni mtetezi mkubwa wa haki za watumiaji wa madawa ya kulevya aina ya marijuana hali iliyosababisha kuzuiwa kuingia nchini Norway baada ya kujaribu kubeba madawa hayo.
Imeandaliwa na Elizabeth Edward wa Mwananchi kwa msaada wa mtandao.
1 comment:
Luka mi nakwambia Huyu bangi tu akuna lolote huyo mtu wanaye muabudu alikataa yeye si mungu an alishakufa long time.... Jamani haile selassie sio king of kings, lion of the tribe of juda or the most high god... Ni mtu tu... Sasa snoop lion amependa jinsi Hawa rasfarians wanavyokula jani Kama Hawana akili nzuri.
Post a Comment