BILA shaka wapenzi wa safu hii ni wazima wa afya na mnaendelea na shughuli zenu za kila siku kama kawaida.
Kama hivyo ndivyo, namshukuru Mungu na niko tayari kwa ajili ya kuwapa darasa maridhawa juu ya tatizo la hisia mbaya ambalo limekuwa likiwatesa watu wengi sana wanapoangukia katika uhusiano.
Kabla ya kupiga hatua nyingi nachukua fursa hii kuwaomba radhi wasomaji waliojiandaa kwa mada ya wanawake wenye lengo la kuolewa mapema iliyotambulishwa wiki iliyopita katika safu hii, itawajia siku za usoni.
Kabla sijaongeza spidi na kuanza kuchambua vipengele kadhaa vya mada hii kwa undani, niwape utangulizi ambao utawaweka sawa katika somo hili linaloweza kukuweka sawa.
HISIA NI NINI?
Siku zote uhusiano wa kimapenzi kati ya mwanamke na mwanaume hutawaliwa na hisia. Zipo hisia za aina nyingi lakini kimsingi zimegawanyika katika mafungu mawili. zaweza kuwa nzuri au mbaya.
Hisia ni hali ya mtu kuwa katika hali fulani ya kuamini kile anachokiamini na hataki kugeuka nyuma.
Hisia nzuri hudumisha mapenzi ya wawili wanaopendana kwa dhati. Unapozipeleleka hisia zako kumuwazia mpenzi wako mambo mazuri halafu na yeye ukakuta amelala katika mawazo yako, hakika mtaenda sawa. Penzi lenu litadumu.
ANGALIZO
Ni vyema kuwa na hisia nzuri kwa mpenzi wako hata kama itatokea bahati mbaya ukakuta tofauti na ulivyokuwa ukiwaza kuliko kutanguliza kuwa na hisia mbaya bila kuwa na uhakika na kile kilichomo mawazoni mwake.
Marafiki zangu, nisiwachoshe sana kwa kuzungumzia hisia moja, kwani kwenye hisia nzuri hakuna matatizo mengi kama ilivyo kwenye hisia mbaya. Hisia mbaya huharibu mapenzi ya kweli, husababisha migongano, malumbano na hata kuvunja kabisa uhusiano kama siyo ndoa.
Ndugu zangu, wapenzi wengi wamejikuta wakiingia katika migogoro inayopelekea ndoa/ uhusiano kuvunjika kwa sababu ya kuwatawaliwa na hisia mbaya kwa wenza wao.
Utakuta mtu anakosa imani na mwenzake, kisa kikiwa ni kuchelewa kurudi nyumbani.
Moja kwa moja anaanza kufiria kuwa atakuwa amepitia kona, ataanza kumchunguza na kutafuta kitu kinachoweza kumfanya ampate na kosa la kuweza kumuhukumu.
Hata ule uchangamfu ambao amekuwa nao siku zote, unatoweka kama samri iliyokwa kwenye kikaaongo kilichowekwa jikoni.
Yaani tatizo dogo linamfanya mtu kupeleka hisia zake mbali na kuanza kujiuliza maswali na kujijibu kwa kutumia hisia zake.
Ukichunguza kwa undani utagundua kimsingi yote anayowaza yanakuwa hayana ukweli wala kufanana na uhalisia.
Hisia tu zinamfikisha mtu mahali aanze kusema labda pengine mpenzi wake alipitia ‘chobingo’, atakuwa na mtu mwingine, amenisaliti na mengine mengi ya sampuli hiyo.
CHANZO NI NINI?
Marafiki zangu, katika makala haya tutapata kujua sababu na tiba tatizo hilo la kuwa na hisia mbaya kwa mwenzako.
Kuna vitu vingi ambavyo vinazungumzwa kuwa ni chanzo cha mmoja kutokuwa na imani na mwenzake.
Kama hivyo ndivyo, tuanze kwa kuzitazama baadhi ya sababu zinazopelekea mpenzi kuwa na hisia mbaya kwa mwenzake.
1.Tabia yako mbaya
Siku zote mwizi hawezi kuwa na imani na mwenzake. Hivyo mara nyingi mtu hukosa imani kwa mpenzi wake kwa sababu yeye mwenyewe huwa ana tabia ya kumsaliti mwenzake. Hisia zake huwa mbaya kwa mpenzi wake hata kama mwenzake hayupo hivyo anavyomfikiria.
2.Wivu
Wivu huwa ni mzuri lakini wakati mwigine ni mbaya. Unapokuwa na wivu wa kupitiliza, matokeo yake ni kuanza kumhisi mwenzako vibaya. Mtu anakuwa na wivu kiasi ambacho anatamani kila mpenzi wake anapokwenda na yeye awepo pembeni. Asipomuona mpenzi wake kwa saa moja anaanza kumhisi vibaya.
3.Kutojiamini
Ndugu zangu, imani siku zote hujengwa na nafsi ya mtu. Mtu anapokosa imani ya kujikubali, basi huanza kuhamishia lawama kwa mwenzake. Hapa mtu anashindwa kujiamini kama anaendana na mpenzi wake. Anajitathimini kisha anajikosoa na kujiona yeye siyo wa kuweza kuwa na mpenzi kama huyo aliyenaye.
Anaweza kuhisi labda hawaendani kwa utajiri, mtu anaweza kujipima uwezo wa kimavazi na vitu vingine vyenye thamani.

www.globalpublishers.info
1 comment:
Weeee hayaaaa weeeee....nimekupata kwa herufi kubwa msg delivered. Zote zipo kwangu sikatai ila ya kwanza naikataaa kabisaaa.
Post a Comment