ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 11, 2012

USAFI WA VIONGOZI NDANI YA CHADEMA WATIWA DOA, KIGOGO WAKE AHUSISHWA NA UJANGILI



CHADEMA wameumbuka baada ya kigogo wa chama hicho kutuhumiwa kwa kujihusisha na ujangili huku, Mbunge wake wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, akipelekwa kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kutokana na kauli ya uchochezi na kulidanganya bunge.

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema bungeni jana mjini hapa kuwa, kutokana na kauli ya uzushi aliyotoa Msigwa, analipeleka suala laked kwenye kamati ya hiyo kuchunguzwa.

Hatua hiyo ilitokana na Msigwa, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii, kumtaja Mzee Lazaro kuwa anamiliki bunduki aina ya Refle na kwamba anatuhumiwa na ujangili.

Msigwa alisema Mzee Lazaro ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), wilaya ya Karatu mkoani Arusha jambo ambalo si la kweli.

Kauli hiyo ilimfanya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) William ukuvi,kusimama na kumtaka Msigwa kudhibitisha madai hayo.

“Namheshimu sana Mchungaji, lakini kutokana na kanuni ya 64 (1) kuhusisha vitendo vya mtu na serikali si sahihi. Pia serikali sio zembe na dhaifu, Naomba atoe udhibitisho wa ujangili wa Mzee Lazaro,” alisema.

Hata hivyo, Mnadhimu Mkuu wa kambi ya Upinzani, Tundu Lisu, alisimama na kuomba mwongozo wa Naibu Spika kwa kutumia kanuni ya 63; kwamba mtu anayedaikauli iliyotolewa ni ya uongo anapaswa aithibitishe.

“Kwa mujibu wa kanuni ya 63 (4), Mheshimiwa Lukuvi anatakiwa kudhibitisha kwanza uongo na ndipo msemaji wa kambi ya upinzani naye athibitishe madai hayo,” alisema. Hata hivyo jioni, Lukuvi alisima na kuthibitisha kauli yake kwa kusema Msigwa amelidanganya bunge.

"Kanuni inakataza kutaja majina ya watu ambao si wabunge na kwa kuwa amemtangaza Mwenyekiti wa CCM Kararu anaitwa Mzee Lazaro napenda kusema kuwa tarifa hii ni ya uongo kwani Mwenyekiti wa CCM Karatu anaitwa John Zakaria Tipa.

Huyo sisi ndio tunaomjua. Hapa Sendeka anamfahamu huyu aliyemtaja yeye ni Mwekekiti wa halmashauri ya Karatu ambayo inaongozwa na Chadema. Jamani tumtangulizeni Mungu, kwani hatutaweza kusema uongo, hivyo namuomba athibitishe kauli au afute kauli yake,"alisema na kuongeza kuwa "Mheshimiwa Naibu Spika, kama Mzee Lazaro Aiyetajwa na Msigwa ni Mwenyekiti basi ni wa Halmashauri na wilaya ya Karatu na ni wa CHADEMA.

Alisema Oktoba 10, 2010, watu saba walikamatwa wakiwa na gari la serikali lenye namba za usajili SM 4117 linalotumiwa na Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye ni wa CHADEMA.

Lukuvi alisema diwani wa CHADEMA wa kata ya Lotiya na askari Idara ya Wanyamapori walikamatwa wakiwa na silaha aina ya Refle ikiwa na risasi saba. Kwa mujibu wa Lukuvi, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Karatu anaitwa John Zakaria Tippa na huyo anayeitwa Mzee Lazaro ni Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ambaye anatokea Chama cha Chadema.

Alisema Mwenyekiti wa CCM wa wilaya hiyo hahusiki kabisa na tuhuma zozote za ujangili, wala hamiliki bunduki na yuko safi.

"Waheshimiwa wabunge, Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Karatu yuko safi kama ilivyo chama chake, hahusiki na kashfa yoyote ile, yanayoelezwa hapa ni uzushi mtupu.

"Hizi ni taarifa za uongo, na omba aliyesema kuwa Mwenyekiti wa CCM wilayani Karatu anaitwa Lazaro athibitishe na afute uongo wake.

"Lazaro kama ni Mwenyekiti basi ni wa Halmashauri na ni wa CHADEMA," alisema.Katika hali isiyo ya kawaida, Msigwa aliwasilisha kwa Ndugai, adendamu ya kusahihisha alichokisema katika hutuba yake, lakini ilipanguliwa kwani alichokisahihisha kilikuwa si sahihi. "Nimepata adendamu hapa kutoka kwa Mheshimiwa Msigwa lakini alichosahihisha hapa sio sahihi, ameniletea kitu tofauti kabisa, hivyo tunaendelea na shughuli zetu kama kawaida," alisema.

Kwa upande wake, Ndugai, alisema Spika wa Bunge, Anne Makinda, amekuwa akionya mara kwa mara tabia za wabunge kuwataja watu walionje ya bunge kwa vile hawawezi kujitetea.

Alisema jambo hilo si jema na hata mwenyewe amekuwa akikemea jambo hilo mara kwa mara lakini limekuwa likifanywa na baadhi ya wabunge. "Jambo hili tumekuwa tukilionya mara kwa mara mimi na spika lakini limekuwa likishika kasi...hivyo nalipeleka kwenye kamati ya Haki, Maadili ya Bunge, ilitolee uamuzi.

"Ninawaomba wabunge muache chuki na sio kuwa CCM anakuwa adui wako nilazima tuheshimiane na tupendane," alisema. Akitoa hoja ya msingi, Msigwa alidai kuwa Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Karatu, Mzee Lazaro anajihusisha na ujangili.

Alisema Mzee Lazaro anamiliki silaha aina Rifle 375 na ni mshiriki wa mtandao wa ujangili. Msigwa, alisema kuna vielelezo vinaonyesha kuwa Lazaro anashirikiana na Bryson Baloshingwa ambao hadi sasa hawajakamatwa licha ya kufahamika.

"Mheshimiwa Naibu Spika, kambi ya upinzani tunasikitishwa kuona kuwa hadi sasa watuhumiwa hawa hawajachukuliwa hatua yoyote licha ya kufahamika," alisema. Alisema Lazaro ametajwa kwenye orodha ya watu wanaotuhumiwa kwa ujangili wa Tembo.

No comments: