ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, August 12, 2012

WAISLAM WA SPRINGFIELD WAFUTURU NA KUPATA SALA YA ISHA PAMOJA

 Watanzania waishio Marekani katika mji huu wa Springfield Ma kama unavyonekana katika picha, walifuturu na kusali swala ya isha pamoja. Watanzania wa mji huu wa Springfield wamejiwekea utamaduni kama huu wa kukusanyika pamoja na familia zao na kufanya mambo ya kicommunity hasa inavyofikia kipindi kama hiki cha mfungo wa ramadhani. Pata picha na matukio  ambayo yalijiri jioni hiyo huko Springfield kupitia hapa katika blog yako ya vijimambo ambayo ilikuwa live katika sehemu  hiyo ya tukio.
 Akina mama wakipata futari tayari kwa kutaka kufuturu kama wanavyoonekana katika picha
 Chakula kilikuwa cha kutosha kwa wale wanao miss vyakula vya kitanzania hapa ndo palikuwa mahala pake.
 Watoto nao walikuwepo sehemu hiyo wakiwa wamevalia mavazi rasmi ya kiislam
 Hapa ni watoto wa Ustadh Akida wakiwapata ukodak wa vijimambo
 Wanaume wakiwa tayari kwenye line ya kujipatia chakula kwa ajili ya kufuturu kama unavyomuona ustadh Akida mbele ya ukodak wa vijimambo.
 Chakula kilikuwa cha kutosha watu walikula na kutosheka.
 Ustadh Mafutah kutoka New York alikuwepo nae kama mgeni mwalika katika futari hiyo
 Akina baba wakisali swala ya Isha kwa pamoja baada ya kumaliza kufuturu
 Akina mama nao hawakubaki nyuma waliswali nao swala ya isha kama wanavyoonekana katika picha
 Swala ya isha ikiendelea baada ya kumaliza kufuturu
Ustadh Mafutah kutoka New York akitoa mawaidha baada ya swala ya Isha, kwa picha zaidi bofya (ready more)






3 comments:

Anonymous said...

mashalaah mmependeza waislam wa boston kanzu nzuri mmependeza

Anonymous said...

mashallah mungu aendelee kutupa amani na upendo huu inshallah siku moja tujumuike watanzania wote marekani mahala pamoja will be soo nice mungu atujalie.

Anonymous said...

Ameen..Allahu maamin!!