ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, September 27, 2012

*DJ Nijo kufanya ‘balaa’ Sun Ciro kesho Ijumaa*

DJ maarufu kutoka nchini Kenya, Dj Nijo kwa kushirikiana na Dj H’Cue na Dj
Mkali wa hapa nchini, wanatarajiwa kuvurumisha shoo ya aina yake kwenye
ukumbi wa Sun Ciro jijini Dar es Salaam, kesho.

Shoo hiyo maalumu ambayo itapambwa na nyota kadhaa wa hapa nchini,
imedhaminiwa na Kipindi cha ‘Hyped East Africa Show’ kinachorushwa kupitia
king'amuzi cha  Zuku Pay TV,  pamoja na usiku wa flava kali za wiki, ambako
DJ Nijo ataongoza mashambulizi ya kuchezesha ‘cd’ na kuchanganya radha
mbalimbali za muziki.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam  mapema leo, Dj
Nijo alisema kuwa, amejipanga kukonga nyoyo za mashabiki wa burudani
akishirikiana na Madjs wenzake wa Tanzania.

“Kwa pamoja tutakonga nyoyo za mashabiki watakaokuja hiyo kesho Ijumaa
 Septemba 27, 2012,ndani ya Sun Ciro na watashuhudia uwezo wetu na shoo hii
itakuwa ni ya pekee kwa Afrika Mashariki,” alisema Dj Nijo.

Kwa upande wake, Herbart Makusha ‘Dj H’Cue’ alisema kuwa, wamejipanga kutoa
burudani ya aina yake kwa kupiga shoo ya aina yake na ya kwanza kwa Madj
kushirikiana kwa pamoja.

Dj Nijo, pia ameambatana na Dj Imani, ambaye kwa pamoja watachanganya
muziki kwa ustadi mkubwa na kutoa radha tofauti.

Aidha, Meneja wa Fleva za wiki wa Sun Ciro, Dk. Kamaru ‘Dj Mkali, alisema
kwenye shoo hiyo kiingilio kimepangwa kuwa sh 10,000 na ambako kutapambwa
na zuria jekundu (Red carpet) na mastaa wa ndani na nje watapata kupita
humo na kufuruhia shoo hiyo.

Ziara ya Dj Nijo itamalizika kwente ukumbi wa Nyumbani Lounge, kesho,
atakakoangusha shoo vile vile.

Hadi sasa, sho za ‘Hyped East Africa’ zimeshafanywa katika miji ya Malindi,
Embu, Nairobi, Nyeri, Eldoret, Kisumu nchini Kenya na hivi karibuni katika
klabu za ‘Anje Noir’ na ‘Cayenne’ jijini Kampala, Uganda.

No comments: