ANGALIA LIVE NEWS

Friday, September 28, 2012

HIVI NDIVYO WAMACHINGA WALIVYOVAMIA NA KUGAWANA NA KUJENGA VIBANDA VYA KUENDESHA BIASHARA ZAO MJINI ARUSHA JANA!



Vibanda vya wafanyabiashara wadogo (Wamachinga) walivyojenga baada ya
kuvamia na kujipimia maeneo. Hapa vibanda hivyo vinaonekana kuwa tayari
kwa biashara zao.
Wanamama wanaouza mboga mboga ambao walikuwa sehemu ya Wamachinga
waliovamia uwanja huo, wakiendelea na biashara zao baada ya kujigawia
maeneo.
Wamachinga jiji la Arusha
waliokosa eneo kwenye uwanja wa NMC jana wakigawana maeneo baada ya kuvunja
uzio wa bati uliokuwa umezungushiwa kwenye uwanja ambao awali ulikuwa unamikiwa
na Manispaa ya Arusha kabla ya kuuzwa kwa mtu binafsi karibu na Soko la
Kilombero, Kata ya Ngarenaro.
 Wamachinga jiji la Arusha
waliokosa eneo kwenye uwanja wa NMC jana wakigawana maeneo baada ya kuvunja
uzio wa bati uliokuwa umezungushiwa kwenye uwanja ambao awali ulikuwa unamikiwa
na Manispaa ya Arusha kabla ya kuuzwa kwa mtu binafsi karibu na Soko la
Kilombero, Kata ya Ngarenaro.
 Wamachinga jiji la Arusha
waliokosa eneo kwenye uwanja wa NMC jana wakigawana maeneo baada ya kuvunja
uzio wa bati uliokuwa umezungushiwa kwenye uwanja ambao awali ulikuwa unamikiwa
na Manispaa ya Arusha kabla ya kuuzwa kwa mtu binafsi karibu na Soko la
Kilombero, Kata ya Ngarenaro.
 Polisi wakiwa kwenye magari yao
baada ya kufika, kuegesha magari yao upande wa pili wa barabara kwenye kituo cha mafuta kwa
muda, kisha kuondoka bila kutawanya wafanyabiashara wago (Wamachinga) waliovamia na kujitwalia eneo hilo.
Polisi wakiwa kwenye magari yao
wakifika na kuyaegesha magari yao upande wa pili wa barabara kwenye kituo cha mafuta kwa
muda kabla ya kuondoka bila kufanya juhudi zozote za kuwazuia machinga hao
kujitwalia eneo hilo.Picha na Grace Macha-


----

Na Mahmoud
Ahmad-Arusha


 Hali si shwari katika jiji la Arusha na viunga vyake baada ya 
wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga kuzua tafrani mara 
walipovamia eneo la kiwanja cha Ermoil lililopo mkabala na soko la 
Kilombero na kisha kuanza kugawana maeneo ya kufanyia biashara kwa 
kujipimia.

Vurugu
hizo zimetokea jana wakati Rais Jakaya kikwete akiwa jijini Arusha 
kufungua mkutano mkubwa wa mapinduzi ya kijani ambao umehudhuriwa na 
wageni mbalimbali kutoka nchi za Afrika,Amerika,Ulaya na Asia. 

Hatahivyo,katika vurugu hizo mfuasi mmoja wa chama cha     
wananchi(Cuf),Athuman Abrahaman alishambuliwa kwa mawe na kisha 
kujeruhiwa eneo la usoni na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chadema
huku gari la matangazo la Cuf nalo likijikuta likipopolewa kwa mawe 
na spika zake kuharibika vibaya. 

Askari wa jiji la Arusha walionekana majira ya saa 3;30 asubuhi akipita 
na gari lao katika maeneo mbalimbali ya jiji hapa huku wakiwatangazia 
wamachinga wote kuondoka katika maeneo ambayo hayajatengwa kufanyia 
biashara zao.

Askari
hao walikuwa wakiwatangazia wamachinga hao kuondoka katika maeneo 
ambayo hayajatengwa kufanyia biashara huku wakitamka ya kwamba endapo 
wakikahidi watachukua bidhaa zao kwa nguvu na kuwachukulia hatua za 
kisheria. 

Hatahivyo,baada ya muda mfupi ndipo askari hao wali 
anza kutekeleza majukumu yao ya kusomba bidhaa hizo na kisha kuzipakia 
ndani ya gari lao huku wakivipeleka katika ofisi za manispaa ya Arusha.

Hatua
hiyo iliwapelekea wamachinga hao kujikusanya kwa pamoja na kisha 
kuvamia ghafla eneo la wazi wa Ermoil kwa kuvunja uzio wa mabati 
uliokuwepo na kisha kuanza kujigawia maeneo kwa kuyapima kwa kamba. 

Wamachinga hao zaidi ya 200 walivamia huku wengine wakitumia nafasi hiyo
kupora mali mbalimbali zilizopo ndani ya eneo hilo kama mabati,nondo na
saruji zilizokuwa ni mali za mtu anayedaiwa kumiliki eneo hilo. 

Katika heka heka za kugawana viwanja ndani ya eneo hilo wamchinga hao 
walikata miti iliyokuwemo ndani na kisha kuanza kuichoma kwa moto hali 
ambayo ilisababisha wingu zito la moshi kutanda hewani.

Hatahivyo,wakati
tafrani hiyo ikiendelea polisi waliokuwa wamesheheni kwenye magari yao 
walikuwa wakipita mara kwa mara kuzunguka eneo hilo lakini hawakuonekana
wakifanya udhibiti wowote zaidi ya kuwaangalia wamachinga hao. 

Kitendo cha askari wa jeshi la polisi mkoni hapa kushindwa kuwadhibiti 
wamachinga hao kimetajwa kimetokana na uhaba wa askari kutokana na ugeni
wa mkutano wa jana pamoja na kuhofia hali ya amani kuharibika jijini
Arusha.

Mkuu
wa wilaya ya Arusha,John Mongella alilaani tukio hilo na kusema kwamba 
wamachinga hao wamevamia eneo hilo kimakosa kwa kuwa si la kwao huku 
akikitupia lawama chama kimoja cha siasa hapa nchini kwamba kimehusika 
katika kuhamasisha vurugu hizo. 

Alisema kwamba kwa sasa watakutana kujadili tukio hilo kwa undani kwa 
kuwa wana ugeni mkubwa lakini alisema kwamba kitendo cha wafuasi wa 
Chadema kupiga mawe gari la Cuf na mfuasi wake si cha kiungwana.

Kaimu
mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya jiji la Arusha,Omary Mkombole 
alisema kwamba kitendo cha wamachinga hao kuvamia eneo hilo ni kuvunja 
sheria na wataondolewa hapo hivi karibuni. 

Mkombole,mbali na kulaani tukio hilo alisema kwamba uongozi wa jiji 
umepanga maeneo mbalimbali ya kufanyia biashara na eneo hilo ni mali ya 
mtu binafsi ambapo alikuwa ameanza jitihada za kuliendeleza.

Habari na Arusha Yetu

No comments: