Timu ya Kagera Sugar imetishia kuachana na uwanja wanaotumia sasa Kaibata uliopo Bukoba mkoani Kagera kutokana na wamiliki wa uwanja huo ambaoni ni Manispaa ya Mji wa Bukoba kushindwa kuutunza licha ya klabu hiyo kutoa fedha za matengenezo, imefahamika.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Meneja wa timu hiyo, Mohamed Hussen alisema kuwa wameuandikia barua uongozi wa timu hiyo inayomilikiwa na Kiwanda cha Sukari cha Kagera kutaka kuhamia kwenye uwanja mwingine ili kuchezea mechi zao za ligi na tayari wanafikiria kwenda kucheza mechi zao za nyumbani kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Hussein alisema kuwa wanashangaa kuona wamiliki wa uwanja huo wamekuwa wakiutumia katika shughuli mbalimbali huku wakiwaruhusu watu wengine kuutumia uwanja kwa kuchimba mashimo ambayo huhatarisha wachezaji wao na wa timu pinzani wanaofika kucheza mechi za ligi.
"Imekuwa ni tatizo sana siku hizi, tulishiriki katika kutoka fedha za matengenezo ili ligi itakapoanza uwanja uwe kwenye kiwango kizuri lakini imekuwa ni tofauti kabisa, tunakusudia kuuhama kama hali itaendelea kuwa hivi," alisema meneja huyo.
Aliongeza vilevile kuwa wamiliki hao wa uwanja, huku wakifahamu kwamba Kagera Sugar inakabiliwa na mechi mbalimbali za ligi na kirafiki, bado wamekuwa na kawaida ya kuwapa taarifa ya kukodisha uwanja huo kwa taasisi nyingine ndani ya muda mfupi na hivyo kusababisha mabadiliko ya ratiba za mechi zao na kusumbua viongozi wa timu ambao wanakwenda Bukoba wakiwa na bajeti inayokadiria siku maalum za kukaa na si zaidi ya hapo.
Alisema kuwa hadi sasa, tayari wameshawaomba rasmi viongozi wao wakuu kuchukua uamuzi wa kupeleka TFF barua ya maombi ya kuhama uwanja ili wahamishie mechi zao za nyumbani mkoani Shinyanga.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment