Mkurugenzi
wa kampuni ya usafirishaji mizigi nchini uingereza Serengeti,Bw Chris
Lukosi akikabidhi sehemu ya msaada wa vitu mbalimbali kwa mkuu wa mkoa
wa Dar es Salaam Meck Sadiq
Kama tulivyoahidi, leo
tumeukabidhi mzigo wa msaada kutoka kwa watanzania waishio UK kwa ajili
ya kuwachangia wahanga wa mafuriko yaliyotokea jijini Dar.Mizigo hii
imekabidhiwa kwa mkuu wa mkoa wa dar es salaam mheshimiwa Mecky
SadiqMzigo huu tumeusafirisha bure na pia tumeulipia ushuru kama mchango
wetu kwa wenzetu waliopatwa na janga hili.
Mkuu
wa mkoa , kwa niaba ya wanachi wa mabwepande ametoa shukurani kwa wale
wote waliochangia na akatoa mwito kwa wengine kuiga mfano huu wa kutoa.
Sisi Serengeti Freight tunapenda kuwashukuru wale wote waliochangia harambee hii
Pia Tunapenda kutoa shukurani kubwa kwa Jestina George na Urban pulse kwa kushirikiana nasi kukamilisha
zoezi hili
KUTOA NI MOYO WALA SI UTAJIRI
Asanteni sana
CHRIS LUKOSI
No comments:
Post a Comment