TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makore Mashaga, Katibu BFT
Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo nchini, Juliana Yassoda Kesho jumatano atafunga mapamano ya
fainali ya ngumi ya ubingwa wa taifa kwenye uwanja wa ndani wa taifa kuanzia saa tisa
alasiri.
Katika fainali hiyo mabingwa wa kila uzani wataiuka na medali za kwanza za dhahabu na kitita
cha shilingi 30,000 kila mmoja.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mchezo huo nchini (BFT), Makore Mashaga aliliambia gazeti hili
jana kwamba michezo 9 ya wanaume na miwili ya wanawake itachezwa kwenye fainali hiyo ambayo
itawakutanisha mabondia wa uzani wa chini hadi ule wa juu.
Mashaga alisema bingwa wa kila uzani atajinyakulia medali ya kwanza ya dhahabu na pesa
tasilimu Tsh 30,000 kila mmoja huku washindi wa pili wakiondoka na medali ya Fedha na Tsh
20,000 kila mmoja.
"Washindi wa tatu wa kila uzani watapata 10,000 kila mmoja pamoja na medali za Fedha,"
alisema Mashaga na kufafanua kwamba kwa upande wa medali ya tatu washindi ni mabondia wawili
katika kila uzani waliopoteza mapambano yao ya nusu fainali," alisema Mashaga.
Katika mapambano ya jana, Said Hofu wa JKT alitinga fainali baada ya kumpiga Hafidh
Bamtulah, wengine waliongia fainali ni Maulid Athuman Wa Polisi aliyempiga Maro James wa
Ruvuma
Mabondia wengine waliotinga fainali ni Mathar George wa Kilimanjaro atakayezichapa na Ireny
Kimaro wa Tabora kwenye uzani wa light fly wakati Ester Kimbe wa Ngome atatoana jasho na
Mariam Nyerere wa Dodoma katika uzani huo.
Kwa wanaume matokeo ya nusu fainali iliyochezwa jana jioni kati ya Hashim Saimon wa Ngome na
Victor Njaiti wa JKT, Badi Mumbamba wa Temeke dhidi ya Seleman Bamtulah wa Magereza, Mohamed
Chibumbuli wa Magereza dhidi ya Omar Jongo wa Temeke ndiyo yaliamua washindi watakaocheza
fainali ya leo.
Mapambano mengine yalikuwa kati ya Alex Matero wa Temeke dhidi ya Joseph Martin wa JKT,
Yusuph Ndimbo wa Mbeya dhidi ya Shaban Ngaoneka wa Ilala, Yahaya Malik dhidi ya HamAD FURAHISHA.
No comments:
Post a Comment