
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Marekani, Barack Obama na Mkewe Michelle Obama. Wakati wa hafla ambayo Rais Obama aliiandaa kwaajili ya Viongozi Wakuu wa Nchi na Serikali ambao wamekusanyika Jijini New York kuhudhuria Mkutano wa 67 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe anaongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huu akimuwakilisha Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na atauhutubia mkutano huo kwa niaba ya Rais siku ya Ijumaa. Hafla hiyo imefanyika katika Hotel ya maarufu ya Waldorf Astoria jijini New York
No comments:
Post a Comment