Promota Kaike Siraju (kulia) akishuhudia mabondia Fadhiri Majia na Nassib Ramadhan, wakitiliana saini kataba wa kucheza pambano lao lililofanyika June 9, 2012. Promota huyo amedaiwa kuwadhulumu mabondoa chipukizi,Issa Omar na Mwaite Juma hivi karibuni.
Tarehe25/06/2012 aliwasainisha mkataba mbele ya katibu mkuu wa ngumi za kulipwa Tanzania Ibrahim kamwe kuwa Issa omar kucheza na Ramadhan kumbele kwa malipo madogo ya 80,000/=(elfuthemenini), alikadhalika kwa mwaite juma kucheza na Anthony Mathias.
Vijana hao walijiandaa na kucheza kama yalivyokuwa makubaliano na hatimaye Promota huyo kuingia mitini bila ya kuwalipa mabondia hao.
Baada ya pambano alitoroka, Walipojaribu kumdai haki yao kwa siku zilizofuata walipigwa kalenda na kuwatembezatembeza kwa usumbufu kwa kuwaambia wamfuate mara mango garden mara magomeni mara awazimie simu na hatimaye kuwapa neno la kuwakatisha tamaa kuwa waachane naye na kuwatishia.
No comments:
Post a Comment