wananchi wakiwa nje ya ofisi ya chama wanamsikiliza lema
RUFAA ya
kupinga kuvuliwa ubunge wa aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema
(CHADEMA), ambao ulikua inatarajiwa kusikilizwa leo na jopo la majaji watatu wa
Mahakama ya Rufaa chini ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande na wenzake,
Natalia Kimaro na Salum Massatiumesikilizwa ila kesi imearishwa.
Kesi hiyo
ambayo ilikuwa inatolewa maamuzi leo imeairishwa na jaji mkuu wa Tanzania kwa
kile kilichodaiwa kuwa wakili wa upande wa mkata rufaa na wakili wa serekali
kupata matatizo ya kufiwa na baba yao mzazi
Jaji mkuu
alifikia hatua ya kuamua kesi hiyo ihairishwe hadi pale ifikapo October 2 mwaka
huu ambapo ndipo imesemekana huku ya kesi hiyo ndio itakapo tolewa.
Mara baada
ya kesi hiyo kuhairishwa umati mkubwa uliokuwepo mahakamani hapo uliondoka hadi
katika ofisi za chama cha demokrasia na maendeleo Chadema ambapo aliyekuwa
mmbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema alongea na wananchi walikuwa
wakimsindikiza nae aliwasihi wananchi hao kuwaombea majaji wa kesi hiyo ili
waweze kutoa hukumu ya haki.
“mimi sio
kwamba nataka nishinde na wala siogopi kushidwa ila naomba tuwaombe hawa majaji
wa kesi hii ili waweze kutoa maamuzi ya haki yasiyomgandamiza mtu yeyote,na
napenda pia kuchukuwa nafasi hi kuwaeleza kuwa jumanne tunatarajia kufanya
mkutano katika kiwanja cha ngarenaro ambapo hapo ndipo tutakapo fungua kampeni
zetu za udiwani rasmi”alisema lema
Alibainisha
kuwa mbali na kuzindua kampeni pia wanampango wa kuzindua mikutano ambayo
itajulikana kufa au kupana ,mkutano
ambao utafanywa kwa nyumba kwa nyumba
pamoja na kitongoji kwa kitongoji
Hata hivyo, habari za uhakika kutoka mahakamani hapo zinaeleza kuwa tayari mawakili wa pande zote mbili wameandika barua ya kuomba kusogezwa mbele kwa shauri hilo hadi Oktoba 2, mwaka huu, kufuatia mawakili, Tundu Lissu, anayemtetea Lema na kaka yake, Alute Mughwai, anayewatetea walalamikaji, kufiwa na baba yao mzazi.
Shauri hilo lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na wakazi wengi wa Jiji la Arusha na Watanzania wengi linatarajiwa kusikilizwa kwa siku moja kisha kupangiwa tarehe kwa ajili ya kutoa uamuzi.
Wakili Mughwai anashirikiana na wakili Modest Akida kuwawakilisha wadaiwa kwenye shauri hilo ambao ni wanachama watatu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mussa Mkanga, Agness Mollel na Happy Kivuyo, waliofungua shauri lililotengua ubunge wa Lema wakidai kuwa wakati wa kampeni alimdhalilisha mgombea wa CCM, Dk. Batilda Burian kwa kutumia lugha za matusi.
Awali, Lema kupitia wakili wake, Method Kimomogoro, anayesaidiana na Lissu, aliwasilisha kwenye mahakama hiyo hoja 18 za madai akipinga kutenguliwa kwa ubunge wake na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha Aprili 5, mwaka huu.
Kwenye baadhi ya madai hayo, Lema aliiomba Mahakama ya Rufaa kutengua uamuzi wa Mahakama Kuu, uliotengua ubunge wake, huku akiitaka imtangaze kuwa mbunge halali wa Jimbo la Arusha Mjini.
Aidha, aliitaka mahakama hiyo ya juu, iwaamuru walalamikiwa katika shauri hilo walipe gharama za rufaa hiyo pamoja na zile za kesi iliyomalizika kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.
Katika madai mengine, Lema anamlalamikia Jaji Gabriel Rwakibarila, aliyesikiliza kesi hiyo kuwa alitoa uamuzi wake kwa kuzingatia maneno ya uvumi, huku akipuuza ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.
Lema anadai kuwa jaji alikosea wakati alipoamua kuwa mpiga kura yeyote anaruhusiwa kupinga matokeo ya uchaguzi hata kama haki zake za msingi hazijaguswa.

No comments:
Post a Comment