INADAIWA kwamba tofauti na Watanzania wanavyofikiri leo, watu wa Sumbawanga, wengi wao wakiwa wa kabila la Wafipa, walikuwa wanachukia sana uchawi. Katika kuhakikisha wanaishi salama, walitaka kila mtu aliyekuwa akiingia eneo lao ahakikishe anaachana na ushirikina!
Benedict Masai, mwenyeji wa Sumbawanga kutoka kabila la Wafipa anayeishi Dar es Salaam anasema kwamba kila mgeni wa eneo hilo aliambiwa: “Sumba wanga!” ikimaanisha kwamba “Tupa uchawi!”
“Kwa Kifipa neno ‘sumba’ ni tupa na ‘wanga’ ni uchawi,” anasema Masai akizungumza na gazeti hili na kuongeza kwamba kila mtu aliyetaka kuingia Ufipa alitakiwa kuutupilia mbali uchawi wowote aliokuwa nao.
Hivyo, wageni waliokuwa wanaingia Ufipa ndiyo wakatoa jina la eneo hilo wakisema ni eneo la “Sumba wanga”. Hivyo, siku zilivyozidi kusonga mbele, maneno hayo mawili yakawa neno mola la “Sumbawanga” ambao leo ni mji na wilaya katika Mkoa wa Rukwa.
“Ni jina zuri tunalipenda, kwani linaonyesha jinsi tulivyokuwa tunapiga vita uchawi tangu zamani, japokuwa leo hii, mambo yamegeuka na tunaonekana kwamba sisi wenyewe ndiyo wachawi wakubwa,” anasema Masai kwa furaha na huzuni akitaka jina hilo liendelee licha ya kutoa picha mbaya kwa watu wengine.
Habari na GPL
No comments:
Post a Comment