ANGALIA LIVE NEWS

Monday, September 24, 2012

:Waheshimiwa Samwel Sitta,Mark Mwandosya,James Lembeli,Ezekiel Maige,Godfrey Zambi, Joseph Mbilinyi aka Mr II Washiriki Ibada Maalum ya Shukrani iliyoandaliwa na Dk Harrison Mwakyembe iliyofanyika nduli , Ikolo, Kyela


  Mbunge wa Mbeya mjini(CHADEMA)Joseph Mbilinyi aka Mr II-Sugu(kushoto)akisalimiana kwa furaha na Mbunge wa Urambo Mashariki na Waziri wa Afrika Mashariki Samwel Sitt
Mbunge wa mbeya mjini(Chadema)Joseph Mbilinyi aka Mr II -Sugu akiongea na Mwanamuziki mkongwe nchini Mzee king kikii walipokutana  Tukuyu Landmark Hotel tukuyu.Picha na Joseph Mbilinyi-Mbunge wa Mbeya Mjini-CHADEMA

Misa ilifanyika kanisa la nduli , Ikolo, Kyela kwa ajili ya Dr. Mwakyembe akimshukuru Mungu kwa kumponya.Ameamua kujenga kanisa na kituo cha chekechea na biashara za akinamama kama sadaka yake kwa Mungu. Walikuwepo watu wengi akiwemo Samwel  Sitta,Ezekiel maige,Joseph Mbilinyi aka Mr II Tizeba, Mulugo, , Kilufi, Zambi, Mtutura, Mwambalaswa, Mwandosya, Ngoye, Lembeli etc bila kuwasahau Ndg. Mboka - kijana aliyemuokota Dr. Mwakyembe kwenye ajali ya Ihemi Iringa,  pia Ndg Paul Makonda, Rais wa TAHLISO na ambaye anagombea Umakamu Mwenyekiti wa UVCCM, Ndg. Eng Chambo

1 comment:

Anonymous said...

Nikupongeze kwa blog yako, mie natembelea kila siku kujua habari za wenzetu mlioko huko kwa Obama.

Leo hapo juu umeandika Misa, napenda kusema hapa, ni Ibada....jaribu kufanya research utaona Maana ya Misa (Mass) na makanisa gani yanayofanya Misa. Wakatoliki, Anglicana, Lutheran ndio wanafanya misa sababu wanaamini the real presence (Yesu katika Ekarist) hiyo ndio Misa (Do this in Memory of Me)....sisi Pentecost hatuamini hilo, so hii misa unasema ni ya Ibada ya kipendecoste.....ni hilo tu.

Mdau
Mbeya