Mkurugenzi wa Lino International Agency,
Waandaaji wa wa Shindano kubwa la Urembo la Redd’s Miss Tanzania, Hashim
Lundenga (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana
juu ya kuanza rasmi kwa kambi ya Miss Tanzania 2012 pamoja na siku ya fainali
ya Shindano hilo. Kushoto ni Meneja wa Kinywaji cha Redd’s, Victoria
Kimaro na Kulia ni Miss Tanzania 2011, Salha Izrael.
Miss Tanzania 2011,
Salha Izrael (kushoto) akiwa na Mmoja wa washiriki wa Shindano Miss Tanzania
2011, Jennifer Kakolaki.
Mashindano
ya Redds Miss Tanzania kwa sasa yamekamilika katika hatua zote na hatua
ya mwisho ilikuwa hatua ya kanda ambayo kwa sasa imekamilika na
kufanikiwa kuwapata warembo jumla ya 30 .
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam Mkurugenzi wa LINO
INTERNATIONAL AGENCY, Hashim Lundenga alisema mashindano kiujumla katika
ngazi zote hadi kanda yamekuwa na mafanikio makubwa na kuonyesha kuwa
fainali ya Taifa ya mwaka huu itakuwa na ushindani wa hali ya Juu.
Washiriki wengi wa mwaka huu kwa asilmia 90 ni wasomi wanafunzi
wa Vyuo Vikuu na wengine wanatarajia kujiunga na Vyuo Vikuu, jambo
ambalo litaleta hamasa kubwa katika shindano la mwaka huu.
Baada
ya kukamilika kwa mashindano hayo ya Kanda kwa sasa tunatangaza rasmi
kuwa warembo wote 30 walioshinda na kuingia katika kinyang,anyiro cha
Redds Miss Tanzania 2012 wataingia kambini siku ya jumanne October
2,2012 katika Hotel yenye hadhi ya kimataifa ya GIRAFFE HOTEL Iliyopo
hapa Jijini Dar Es salaam,Washiriki hao watakuwa kambini kwa muda wa
mwezi mmoja.
Tunapenda
kuwajulisha wadau wa tasnia ya urembo kwamba shindano la REDDS MISS
TANZANIA 2012 litafanyika siku ya Jumamosi tarehe 03 November 2012
katika Ukumbi wa Hotel ya Blue Peal (Ubungo Plaza).
Kwa
Upande wake Meneja wa Kinywaji cha Redds Original Victoria Kimaro
alisema wao kama wadhamini wakuu wa Redds Miss Tanzania wamejipanga kwa
nguvu kubwa kutoa burudani ya aina yake kwa wadau wote wa tasnia ya
urembo hapa nchini sambamba na kuhakikisha warembo wote waliofanikiwa
kuingia hatua ya fainali watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali.
Kwa kuzingatia
mabadiliko ya Kalenda ya Mashindano ya urembo ya Dunia, Mrembo wa
Tanzania atakuwa na muda mrefu wa maandalizi kwani atatakiwa kuripoti
katika Fainali za Mashindano ya urembo ya Dunia katikati ya mwaka ujao.
2013.
No comments:
Post a Comment