Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Morogoro kasoro uingie dosari, baada ya baadhi ya wajumbe kutaka kuigomea kwa madai ya kunyimwa chai.
Waliotishia kugoma kuingia katika ukumbi wa Magadu, nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro ni wajumbe wa wilaya za Kilombero na Ulanga.
Wajumbe hao waliamua kususia baada ya kutopatiwa kifungua kinywa huku wenzao wa wilaya nyingine wakipewa huku wenyewe wakiambia wasubiri.
Mmoja viongozi wa wastaafu ambaye alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Ulanga, Fadhil Liliguda, alisema baadhi ya vijana hao walitaka kususia uchaguzi huo baada kuwambiwa wasubiri ili mkutano ufunguliwe, lakini walikaidi.
“ Baadhi ya vijana si wastaarabu, kama wameweza kusafirishwa kwa mamilioni kutoka walipokuwa inakuwaje washinde kupewa chai,” alisema Liliguda.
Mwenyekiti UVCCM aliyemaliza muda wake, Jonas Nkya, alithibitisha kuwepo kwa hali hiyo na kueleza kuwa kulisababisha na upugufu wa fedha, lakini walitatua tatizo hilo.
“Jumuiya yetu haina fedha, tumejaribu kuwaomba viongozi wakiwemo mawaziri na wabunge, lakini hakuna aliyetupatia msaada, nyingi nimetoa mfukoni mwangu na marafiki zangu kunichangia tulikuwa na asilimia 30 ya fedha,” ” alisema Nkya.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment